Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
412 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
B. Upande wa ndani wa uinjilisti: kufanya ujumbe wa Habari Njema kuwa wazi kwa kila watu katika lugha na utamaduni wao.
1. Kile tunachoamini na kukiri, Rum. 10:8-13.
2. Umuhimu wa mjumbe, Rum. 10:14-15.
Hitimisho • Wokovu ni ukombozi wa Mungu kwa wanadamu na uumbaji dhidi ya nguvu za shetani na athari za dhambi. • Kupitia imani katika Yesu Kristo, waamini wanakombolewa kutoka kwenye utawala na udanganyifu wa Shetani. • Ukombozi wa Mungu katika Kristo pia huwakomboa waamini dhidi ya athari za Laana na dhambi kwa nguvu za Roho Mtakatifu. • Uinjilisti ni tangazo la ukombozi wa Mungu ulioahidiwa na kutabiriwa kupitia Yesu Kristo kwa ulimwengu wote kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Maswali yafuatayo yalikusudiwa kukusaidia kupitia maudhui ya video. Kuelewa uhusiano wa kina kati ya uinjilisti, wokovu, na ukombozi kutaathiri sana namna unavyoelewa na kuifanya huduma ya kibiblia kwa waliopotea. Toa majibu yako kwa uwazi na kwa ufupi na ikiwezekana yaunge mkono kwa Maandiko! 1. Kulingana na Maandiko, ni sababu gani hasa iliyomfanya Yesu aje ulimwenguni? Ni kwa jinsi gani kifo cha Yesu msalabani kilipokonya uwezo wa wafalme na wakuu wa giza wa kuendeleza udhalimu wao dhidi yetu? 2. Protoevangelium ni nini na kwa nini ni muhimu sana kwa ufahamu wetu wa uinjilisti kama kutangaza ujumbe wa ukombozi wa Mungu dhidi ya ukandamizaji wa kishetani? 3. Maisha ya Yesu yana umuhimu gani kuhusiana na uharibifu wa adui? Jibu kwa uwazi na kwa ufupi. 4. Je, kifo cha Yesu kilitimizaje ukombozi wa wanadamu kutoka kwenye nguvu za shetani, hasa hofu yetu ya kifo na utumwa tunaoteseka nao kutokana na hofu hiyo?
2
U T U M E K A T I K A M I J I
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker