Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | U I NJ I L I S T I NA V I TA YA ROHON I : KUFUNGWA KWA MTU MWENYE NGUVU / 413
5. Ni kwa njia gani ufufuo wa Yesu unatupatia uhakika kwamba ukombozi alioupata unakubaliwa na Mungu hakika? 6. Maandiko yanafundisha nini kuhusu kifo cha Yesu kama adhabu tosha kwa dhambi zetu? 7. Kwa nini waamini hawapaswi kamwe kuogopa utawala wa kishetani tena? Kifo na ufufuo wa Yesu vilimfanya nini Shetani kwa faida ya wanadamu? 8. Roho Mtakatifu anatuhakikishia vipi kwamba katika enzi hii hatuko tena chini ya nguvu za dhambi? 9. Ni wakati gani sisi tunaoamini hatimaye tutakombolewa kutoka katika uwepo wa dhambi? 10. Eleza ni kwa namna gani uinjilisti ni tamko la habari njema ya ukombozi wa Mungu kwa wale wasioamini akiwatoa kutoka katika utumwa Shetani na dhambi. Somo hili linaangazia dhana za msingi zinazotengeneza msingi wa uelewa wetu wa Uinjilisti na Vita vya Rohoni. Uinjilisti hauanzii na kile tunachofanya katika maisha yetu na ushuhuda wetu kwa waliopotea; ulianza karne nyingi zilizopita wakati shetani na wenzi wa kwanza wa kibinadamu walipoasi utawala wa haki wa Mungu. Katika kutafuta kuishi kwa uhuru mbali na mamlaka na utawala wa Mungu, ulimwengu uliingizwa katika machafuko ya kiroho na giza. Sasa, ulimwengu uko katika vita vya kiroho na Mungu ambaye aliahidi kututumia Mwokozi ambaye angeponda kichwa cha nyoka na kuwakomboa watu wake kutoka katika dhambi zao. Yesu Kristo ndiye Mkombozi huyo! Kuelewa mambo haya ya msingi ni muhimu ili kujua kile ambacho uinjilisti unatafuta kufanya na kile ambacho Mungu anafanya wakati wale waliopotea wanapoamini habari njema ya Injili. • Biblia inafundisha kwamba wokovu ni tendo la Mungu kumkomboa mwanadamu na uumbaji kutoka katika nguvu za shetani na matokeo ya dhambi. • Kupitia imani katika Yesu Kristo, wale wanaoamini wanaweza kukombolewa kutoka chini ya utawala wa Shetani na kutoka katika udhalimu wake (udanganyifu na ukandamizaji wake) na hofu ya kifo. • Wokovu wa Mungu katika Kristo pia huwakomboa wale wanaoamini dhidi ya athari za laana na dhambi kwa nguvu za Roho Mtakatifu.
UHUSIANISHAJI
2
Muhtasari wa Dhana Muhimu Ukurasa wa 179 6
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker