Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

414 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

• Uinjilisti ni tangazo la ukombozi wa Mungu kwa ulimwengu wote, ukombozi ulioahidiwa na kutabiriwa kwa njia ya Yesu Kristo katika uwezo wa Roho Mtakatifu.

Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu mgogoro wa kiroho ambao ulitokea kama matokeo ya Anguko, na wokovu kama ukombozi kutoka kwenye mikono ya shetani na dhambi. Dhana hizi ndio msingi wa majadiliano yote kuhusu huduma, uinjilisti, na ukombozi wa kiroho. Je, una maswali gani maalum kwa kuzingatia yale ambayo umesoma hivi punde? Pengine baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. • Kwa nini ni muhimu kuthibitisha tangu mwanzo kwamba Anguko, Laana, na madhara yote ya dhambi vilitokana na uasi wetu na si kwamba ni uumbaji wa Mungu.? • Ni kwa njia gani tunaweza kueleza maovu yote katika historia ya wanadamu kuwa ni matokeo ya ushawishi wa kishetani na pia uchaguzi wa wanadamu kukataa kuishi chini ya utawala wa haki wa Mungu? • Kwa kuzingatia yale tunayojua kuhusu utumwa ambao uumbaji na wanadamu wanateseka nao kama matokeo ya dhambi, kwa nini Yesu pekee ndiye anayeweza kuleta ukombozi kwetu? Thibitisha jibu lako kwa Maandiko. • Je, ni haki kwa Mungu kuwaadhibu wanadamu wote kwa ajili ya dhambi iliyofanywa na Adamu na Hawa? Je, kuna uhusiano gani kati ya kutenda kwako dhambi na anguko lao? • Je, kuuelewa wokovu kama ukombozi kutoka kwenye nguvu za uovu kunaathiri vipi namna tunavyofikiri kuhusu kushirikisha wengine Habari Njema katika uinjilisti? Je, tunapaswa kutarajia nini watu wanapokubali habari njema ya wokovu katika Kristo? • Je, mkristo anawezaje kuuishi kwa ushindi ukombozi ambao

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi Ukurasa wa 179  7

2

U T U M E K A T I K A M I J I

Yesu alimshindia pale msalabani? Ikiwa mwamini haishi katika uhuru wa Kristo, tunaweza kuzungumziaje kile kinachoendelea katika hali yake?

MIFANOHALISI

Demonic Deception Versus Personal Responsibility Katika kutoa ushauri nasaha kwa familia ambayo mpendwa wake alikuwa ameingia kwenye matatizo na sheria na mahakama, suala fulani linaibuka kutoka kwa mwanafamilia mmoja kuhusu ushawishi wa shetani katika maisha ya mpendwa huyu. Anaamini kwa moyo wake wote kwamba udanganyifu na ushawishi wa shetani

1

Ukurasa wa 180  8

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker