Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | U I NJ I L I S T I NA V I TA YA ROHON I : KUFUNGWA KWA MTU MWENYE NGUVU / 415
ndio kiini cha kile ambacho kimetokea kwa mpendwa wao. Ni ushawishi wa kipepo pekee ndio ungeweza kuwa ufafanuzi pekee wa kukengeuka kwake, kukubali kwake marafiki wabaya kama hao, na kujihusisha kwake katika uhalifu na jeuri. Wanafamilia wengine wanakataa maoni hayo, wakisema kwamba mpendwa wao alijua lililo sahihi, lakini aliamua kupuuza mafundisho mema ya nyumbani na kufuata njia ya marafiki zake wa mtaani wasio na nidhamu wala malezi. Je, unaweza kuelezaje kwa familia hii uhusiano kati ya udanganyifu wa shetani katika maisha yetu na uchaguzi wetu binafsi wa kufanya makosa kama sababu ya dhambi zetu binafsi? Usitarajie Badiliko kwa Haraka Katika kikao kabla ya utafiti wa jumuiya/kampeni ya nyumba kwa nyumba, mmoja wa wazee anatoa neno la kuwatia moyo watendakazi kabla ya kuondoka kanisani. Katika kuwaomba wasivunjike moyo, anadokeza kwamba tunapaswa kuwashirikisha jirani zetu Injili, tukiwaombea kwamba Mungu afanye kazi maishani mwao, lakini tusiwe wenye kutarajia sana mabadiliko ya haraka katika maisha yao. Hata wakisema ndiyo kwa Kristo, badiliko la maadili linahitaji wakati na jitihada nyingi. Baadhi ya watendakazi wanakataa maoni haya, wakisema kwamba tunaweza kutarajia mabadiliko makubwa kila wakati mtu anapomkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi. Je, ni jibu gani sahihi/bora/la kibiblia zaidi kwa mjadala huu? Si Makosa Yetu Katika kujadiliana na baadhi ya vijana mtaani kuhusu Habari Njema na wokovu, mmoja wa vijana hao anakataa wazo la kwamba mitaa iko katika hali ngumu kwa sababu ya dhambi zetu. Anadokeza, “Kwa miaka mingi, nchi hii iliwachukulia watu ambao si weupe kama daraja la pili, bila kuturuhusu kupiga kura, au kufanya kazi, au kushiriki katika jamii pana zaidi. Hatukuomba kuishi kwenye mitaa hii, na hakuna mtu yoyote anayeishi humu, kama angeweza kupiga kura juu ya jambo hili, angetaka kuishi katika mtaa ambao watu wetu hawako salama, hawali vizuri na hawana mavazi, hawana kazi nzuri na wala hawana vitu vizuri kama kila mtu mwingine. Sijali unachosema! Sio kosa letu kwamba mambo yako hivi. Jamii haijawahi kututendea haki – wao ndio wametufanya tuwe hivi!” Je, ungejibuje mtazamo huu?
2
2
U T U M E K A T I K A M I J I
3
Tatizo LikoWapi? Baada ya kujifunza wazo zima la Biblia la wokovu kama ukombozi, mmoja wa wanafunzi darasani anaibua swali muhimu. “Tunaweza
4
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker