Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
416 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
kuahidi ushindi wa aina gani kwa watu ambao wamekuwa wakiishi maisha yao kwa miongo kadhaa wakifanya kila aina ya mambo haramu na yasiyo ya maadili? Nimefanya kazi kwa miaka mingi katika programu ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya ambapo tumeshirikishana habari za Bwana na wanufaika wa programu husika, na watu wengi wameonyesha kwamba wamemwamini Kristo. Hata baada ya kufanya ukiri huo, wanaendelea kutumia dawa za kulevya, kucheza kamari, kushiriki katika kila aina ya mambo ambayo najua hayampendezi Bwana. Tunawezaje kusema kwamba wokovu ni ukombozi wakati watu wengi sana wanaodai kuokolewa hawaishi maisha yaliyojaa ukombozi na uhuru?” Je, unawezaje kuelezea kweli hizi? Ingawa Mungu aliumba ulimwengu ukiwa mwema na huru, ulianguka katika giza na machafuko kwa sababu ya kutotii kwa shetani na wanadamu wawili wa kwanza, Adamu na Hawa. Kama matokeo ya Anguko hili, nguvu za kipepo ziliachiliwa katika ulimwengu, viumbe vyote viliwekwa chini ya Laana na utumwa na uharibifu, na wanadamu waliwekwa chini ya ubinafsi, mateso, na kifo. Sasa kupitia kifo na ufufuo wa Yesu Kristo, ukombozi wa Mungu dhidi ya shetani na madhara ya dhambi umetujilia. Katika Yesu tumekombolewa kutoka kwenye adhabu ya dhambi, tunakombolewa na Roho Mtakatifu kutoka kwa roho ile (yaani, Ibilisi) na nguvu za dhambi, na hivi karibuni tutakombolewa dhidi ya uwepo wa dhambi katika Ujio wa Pili wa Yesu. Uinjilisti ni kutangaza ukombozi huu kupitia habari njema ya Injili ya Kristo. Kama ungependelea kufuatilia baadhi ya mawazo ya Vita vya Kiroho: Kufungwa kwa Mtu Mwenye Nguvu , unaweza kutaka kujaribu vitabu hivi: Billheimer, Paul. Destined for the Throne . Minneapolis: Bethany House, 1975. Epp, Theodore H. The Believer’s Spiritual Warfare . Lincoln: Back to the Bible, 1973. Hayford, Jack W. (Executive Editor). Answering the Call to Evangelism (Spirit-Filled Life Kingdom Dynamics Study Guides). Nashville: Thomson Nelson Publishers, 1995. Sasa ni wakati wa kujaribu kutenga kanuni au dhana ambayo inaweza kukusaidia katika hali yako maalum ya huduma. Tafiti mawazo, dhana, na kweli mbalimbali ambazo zimetambulishwa katika somo hili, na elekeza umakini wako kwenye ufahamu mmoja ambao utatafakari na kuuombea katika wiki hii yote ijayo. Je, ni wazo gani
Marudio ya Tasnifu ya Somo
2
U T U M E K A T I K A M I J I
Nyenzo na Bibliografia
Kuhusianisha Somo na Huduma
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker