Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | U I NJ I L I S T I NA V I TA YA ROHON I : KUFUNGWA KWA MTU MWENYE NGUVU / 417
maalum ambalo Roho Mtakatifu amesisitiza kwenye moyo wako kuhusu uinjilisti, vita ya kiroho, na wito wako maalum wa uinjilisti katika jamii yako? Ni hali au mazingira gani hasa yanayokuja akilini unapofikiria namna Mungu alivyoahidi ukombozi kwa wale wanaoamini Habari Njema? Je, ni kwa jinsi gani Mungu anataka mawazo yako mwenyewe yabadilike kulingana na ukweli ambao umesikia pamoja na wanafunzi wenzako juma hili? Mwombe Bwana akupe hekima unapoomba na kutafakari mada hii ya somo na ukweli ambao Roho amekusisitizia katika somo hili. Katika namna maalum kabisa omba ili Bwana akupe utambuzi na uelewa wake unapotafuta kuuelewa uinjilisti katika muktadha wa wokovu kama ukombozi kutoka katika nguvu za shetani na kutoka katika dhambi na athari zake. Mwombe Mungu akuongezee imani yako kwa matokeo, akupe utambuzi mpya wa Injili kama uweza wa Mungu uletao wokovu kwa wote waaminio (yaani, Warumi 1:16). Omba upako wa Roho unaposhirikisha wengine Habari Njema ili nguvu ya wokovu wa Mungu iweze kujidhihirisha katika maisha ya wale unaowashirikisha, kama nguvu hiyo hiyo inavyoendelea kubadilisha maisha yako mwenyewe katika Kristo.
Ushauri na Maombi
2
KAZI
U T U M E K A T I K A M I J I
Waefeso 2:8-10
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/ books ili kujua kazi ya kusoma ya juma lijalo, au muulize Mshauri wako.
Kazi ya Usomaji
Kwa mara nyingine, hakikisha kwamba umesoma kazi zilizo hapo juu, na kama wiki iliyopita, ziandikie muhtasari mfupi na ulete muhtasari huo darasani wiki ijayo. (Tafadhali ona “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” katika ukurasa wa 16). Kadhalika, sasa ndio wakati wa kuanza kufikiria kuhusu muktadha wa kazi yako ya huduma kwa vitendo, na pia kuamua ni kifungu gani cha Maandiko utakachochagua kwa ajili ya kazi yako ya ufafanuzi wa Maandiko (eksejesia). Usichelewe kufanya maamuzi juu ya kazi yako ya huduma na ile ya ufafanuzi wa Maandiko. Kadiri unavyofanya maamuzi mapema, ndivyo utakavyopata muda wa kutosha kujiandaa!
Kazi Zingine Ukurasa wa 180 9
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker