Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 3 | MKAZO KUHUSU UZAZ I : UKUA J I WA KAN I SA / 419
Mkazo kuhusu Uzazi Ukuaji wa Kanisa – Kuongezeka katika Idadi na Ubora
S OMO L A 3
Ukurasa wa 183 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maudhui ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuonyesha kutoka kwenye Biblia namna ufuasi wa kina unavyozaliwa na kuthibitishwa katika jumuiya ya Kikristo. • Kuelezea hatua tatu jumuishi za upandaji kanisa mijini: kuinjilisha waliopotea, kuwaandaa wanafunzi wapya kuishi maisha ya Kikristo katika muktadha wa jumuiya ya Kikristo - Kanisa, na kuwawezesha viongozi na jumuiya kujizalisha na kushirikiana na makanisa mengine yenye nia moja. • Kuangazia kanuni kumi muhimu zinazotolewa kutoka kwenye kielelezo cha upandaji kanisa kutoka kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, na kuzitumia katika juhudi zako za upandaji kanisa mjini. Imetupasa Kumtii Mungu KulikoWanadamu Mdo. 5:27-32 – Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza, 28 akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu. 29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. 30 Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. 31 Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi. 32 Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio.” Je, ni kwa mamlaka ya nani tunayo haki ya kuzungumza na wale ambao hawaamini madai ya “kigeni” ya Yesu wa Nazareti? Katika nyakati hizi za usahihi wa kisiasa na wakati ambapo kutokuwepo ustahimilivu wa kidini kunazaa vitendo vya kutisha vya vurugu na ugaidi, je, watu wote wenye maadili hawapaswi “kujishusha chini,” na kuruhusu kila mtu aamini tu kile anachoamini, bila kuingilia au kuhukumu? Je, wakati wa kushirikisha imani yako kwa madhumuni
Malengo ya Somo Ukurasa wa 184 2
3
U T U M E K A T I K A M I J I
Ibada Ukurasa wa 184 3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker