Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

420 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

ya kuwashawishi wengine kufuata mtazamo wako ni wa kizamani, uliopitwa na usio sahihi? Mfano wa Mitume ni wenye kufundisha kwa wanaume na wanawake wote walioitwa kuwakilisha maslahi na sifa ya Bwana wetu mfufuka mbele ya wengine. Licha ya upinzani wa kutisha na tishio la madhara makubwa ya kimwili ikiwa wangeendelea kushirikisha wengine habari njema ya Kristo na Ufalme wake, Mitume hawakutetereshwa. Petro na Mitume wako wazi mbele ya vitisho: “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi. Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio.” “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.” Agizo Kuu la Bwana wetu, ingawa lilitolewa kwa kundi la mashahidi wenye ari waliosikia amri ya Bwana mfufuka ya kwenda ulimwenguni kote na kuhubiri Habari Njema, ni amri ya vizazi. Hata atakapodhihirika Bwana wetu, kila kizazi cha Kikristo kinaenda na Injili ya Ufalme katika Yerusalemu yake, Yudea na Samaria. Sisi sote tunawajibika katika kupeleka Injili hadi miisho ya dunia. Hakuna kitu kinachoweza kutuzuia au kututisha, kwa maana Yesu yule yule wa Nazareti aliyesulubiwa Yerusalemu karne nyingi zilizopita ameinuliwa. “Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.” Akiwa ameinuliwa mkono wa kuume wa Mungu kama Kiongozi na Mwokozi, sasa toba na msamaha vinahubiriwa kwa ulimwengu wote. Katika hili, Mitume na Roho Mtakatifu wanashuhudia. Msingi wa huduma yetu ni nini? Kwa nini tunaweza kubaki bila kutikiswa tunapokabiliana na mateso makali na kukataliwa? Kwa nini tunapaswa kwenda, hata kama hakuna mtu anayeitikia? Mungu wetu amemwinua Masihi kuwa Bwana na Mwokozi, na kwa kutii amri yake, washirika wa Kanisa wamekuwa wakienda kuhubiri kwa karne nyingi. Wengi wamekufa, wengi wameteseka, na wengi wameteswa. Lakini hakuna hata mmoja aliyeshindwa. “Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi. . .”(.) Amiri huyu mkuu atatuongoza hadi tutakapokufa. Hadi wakati huo, imetupasa kumtii Mungu, kuliko wanadamu.

3

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker