Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | MKAZO KUHUSU UZAZ I : UKUA J I WA KAN I SA / 421

Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu, Baba yetu wa mbinguni, uliyedhihirisha pendo lako kwa kumtuma Mwanao wa pekee ulimwenguni ili wote wapate kuishi kwa yeye: ulijalie Kanisa lako kwamba kwa uwezo wa Roho litimize agizo la kuwatangazia watu wote Habari Njema za Yesu Kristo , na kutuimarisha katika azimio letu la kufanya kazi na kushuhudia ufalme wake, kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu. ~ Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. Kitabu cha Mhudumu cha Kutumika Pamoja na Ekaristi Takatifu na Sala ya Asubuhi na Jioni . Braamfontein: Idara ya Uchapishaji ya Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. uk. 114.

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

Pitia upya na mwenzako, andika na/au jikumbushe kifungu cha mstari wa kumbukumbu uliopewa kwenye kipindi cha darasa lililopita: Waefeso 2:8-10.

Mapitio ya Kukariri Maandiko

Wasilisha muhtasari wako wa kazi ya kusoma ya juma lililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache ya mambo makuu ambayo waandishi walikuwa wakitafuta kuyaainisha katika kazi ya usomaji uliyopewa (Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukusanya

3

U T U M E K A T I K A M I J I

KUJENGA DARAJA

Matangazo na Utauwa Vinapaswa Kwenda Pamoja Katika kikao cha viongozi wa kanisa fulani la mjini ambalo lilidhamiria kukua, mmoja wa mashemasi viongozi alitoa maoni kwamba ingawa kanisa lao ni la kimungu, halijui jinsi ya kujitangaza kwa wale walio jirani. “Tuseme ukweli,” alisema, “sababu inayopelekea makanisa mengi katika vitongoji kukua ni kwamba kila mara yanawashirikisha wengine ujumbe na vipindi vyao– wanalitoa neno nje ya mipaka. Na, kilichokizuri kwa bata bukini jike ni kizuri kwa bata bukini dume. Ikiwa tunataka kukua kama kanisa, itabidi tupate mikakati bora ya matangazo. Tunaweza kuanza kidogo, lakini hapo ndipo tunapopaswa kuanzia. Ninaamini, na ninyi pia mnahitaji kuamini kwamba matangazo na utauwa vinapaswa kwenda pamoja.” Je, ndugu huyu yuko sahihi? Matangazo yana nafasi gani katika kukuza Kanisa la Yesu Kristo?

1

Ukurasa wa 185  4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker