Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

422 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Hauko Tayari Bado Hosea ni Mkristo mwenye miaka ishirini na miwili, ana akili na ni Mkristo mzuri ambaye anaonyesha shauku kubwa ya kushirikisha wengine Habari Njema. Asubuhi moja baada ya ibada unamkuta amevunjika moyo. Unapouliza kinachoendelea, anasema kwa huzuni, “Ooh, ni namna ninavyojisikia hivi karibuni. Tangu nilipotoa moyo wangu kwa Bwana takribani miaka miwili iliyopita, nimekuwa na mzigo huu mzito wa kuwa katika huduma ya Bwana. Hakuna siku inayopita bila moyo wangu kuchochewa kuhusu waliopotea. Siwezi kulala, ninalia kila wakati; asubuhi na mapema ninaamka, ninaanza kutembea huku nikimwomba Bwana aniambie anachotaka nifanye. Naamini ameniita kwenye huduma. Nilimshirikisha Shemasi Wilson kuhusu mzigo nilionao, naye akaniambia kwamba sikuwa na umri wa kutosha katika Bwana ili kupewa nafasi ya kuwashirikisha wenigne Injili. Ninahitaji muda zaidi katika Neno na kanisani ili kujiandaa. Najua yuko sahihi, lakini mzigo huu unakaribia kunimaliza. Nifanye nini?” Ungemjibuje Hosea? Kanisa LinazimaWatu Unasikia kuhusu kikundi kipya cha kujifunza Biblia kilichoundwa na washirika wa kanisa ambao wamechukizwa na jinsi mambo yanavyoendelea katika kanisa. Ingawa hawakusudii kuhama kanisa, wala kuongoza kampeni ya kuchukua nafasi ya mchungaji, hawaamini kwamba kanisa linatosha kuwakuza waongofu wapya. Muziki ni wa kizamani, ibada ni kavu, na watu wanaonekana si rafiki. Kikundi hiki kimejiunda kwa nia ya kuwakaribisha na kuwavuta zaidi wanachama wapya. Kama mmoja wa washirika wa kikundi hiki alivyosema hivi karibuni, “Kanisa letu linampenda Bwana na linapenda Neno, lakini lina matatizo fulani. Ninahofia kwamba watu wapya watatuona kuwa ni watu wagumu sana na wasiovutia. Tulianzisha kanisa hili ili kuleta msisimko fulani. Kanisa linazima watu, na tutalisaidia.” Una maoni gani kuhusu maoni ya mwanachama huyu na uundwaji wa kikundi hiki kipya?

2

3

3

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker