Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | MKAZO KUHUSU UZAZ I : UKUA J I WA KAN I SA / 423

Ukuaji wa Kanisa – Kuongezeka katika Idadi na Ubora Jinsi ya Kupanda Kanisa Linalojizalisha Mjini: Muhtasari

Mch. Dk. Don L. Davis

MAUDHUI

Kama wanafunzi walioitwa kutii agizo la Kristo la kwenda na kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi wa Kristo, tunajua kwamba ufuasi wa kina huzaliwa na kuthibitishwa katika jumuiya ya Kikristo pekee. Kupanda makanisa ni kutimiza Agizo Kuu ambalo linahusisha hatua tatu jumuishi: Kufanya Uinjilisti (kuwaokoa waliopotea), Kufuasa (kuimarisha wanafunzi wapya Kanisani), na Kuwezesha (viongozi na kanisa kujizalisha lenyewe katika ushirika na makanisa mengine yenye nia moja). Lengo letu katika somo hili, Jinsi ya Kupanda Kanisa Linalojizalisha Mjini : Muhtasari, ni kukuwezesha kuona kwamba: • Neno la Mungu linafundisha kwamba ufuasi wa kina huzaliwa na kuthibitishwa katika muktadha wa jumuiya ya Kikristo pekee. • Ili kutimiza Agizo Kuu la Bwana Yesu mfufuka lazima tupande makanisa yenye afya, yanayomheshimu Kristo miongoni mwa watu wote wa dunia. • Upandaji kanisa unajumuisha hatua tatu za pamoja za huduma ya ufalme. • Hatua ya kwanza ni Kufanya uinjilisti , tunapowahubiria waliopotea habari njema ya Ufalme katika Yesu Kristo kwa kuwashirikisha neno na kwa matendo. • Hatua ya pili ni Kufuasa , ambako ni kuwaimarisha wanafunzi wapya kuishi maisha ya Kikristo katika mazingira ya jumuiya ya Kikristo – Kanisa. • Hatua ya tatu ni Uwezeshaji , ambao unahusisha kuwapatia rasilimali na kuwaandaa viongozi na kusanyiko la kanisa jipya lililoanzishwa ili kujizalisha na kushirikiana na makanisa mengine yenye nia moja. • Zipo kanuni kumi muhimu za kutuongoza katika juhudi zetu za upandaji kanisa, kanuni ambazo zimetolewa kutoka kwenye huduma ya kitume katika Matendo ya Mitume, na zinaweza kutumika kwa urahisi kwenye juhudi zetu za upandaji makanisa mjini. • Kwa kufanya uinjilisti kwa waliopotea, kuwafuasa Wakristo wapya wapate kukua kama wanafunzi wa Yesu, na kuwawezesha viongozi na makanisa kujizalisha, tunaweza

Muhtasari

3

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker