Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
424 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
kuona makanisa mengi imara na yenye afya yakipandwa katika miji ya taifa letu na dunia nzima.
I. Fanya Uinjilisti: Enenza Habari Njema za Kristo na Ufalme Wake katika Jamii.
Muhtasari wa Maudhui ya Video
Mk. 16.15-18 – Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”
Kazi yetu ya huduma inajengwa juu ya kazi yaMitume. “Wale Kumi na wawili walichaguliwa ili wawe pamoja na Kristo (Mk. 3:14), na ushirika huu uliwapa sifa ya kutenda kama mashahidi wake (Mdo. 1:8); tangumwanzo walijaliwa uwezo juu ya pepo wachafu namagonjwa (Mt. 10:1), na nguvu hii ilihuishwa na kuongezwa, kwa namna ya jumla zaidi, wakati ahadi ya Baba (Luka 24:49) ilipowajia katika kipawa cha Roho Mtakatifu (Matendo 1:8); katika safari yao ya kwanza ya umisheni walitumwa kuhubiri (Mk. 3:14), na katika utume mkuu waliagizwa kufundishamataifa yote (Mt. 28:19). Hivyo walipokeamamlaka ya Kristo ya kueneza injili kwa ujumla. Lakini pia waliahidiwa kazi mahususi zaidi kama waamuzi na watawala wa watu waMungu (Mt. 19:28; Lk. 22:29-30), wakiwa na uwezo wa kufunga na kufungua (Mt. 18:18), kuondoa na kufungia dhambi (Yn. 20:23) .” ~ D. R. W. Wood. New Bible Dictionary . Toleo la 3. Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1996. uk. 202.
A. Umuhimu wa Uinjilisti katika kuzidisha makanisa ya mijini
1. Uinjilisti ni kitovu cha utume na uenezi wote wa Kikristo; Habari Njema ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa wote waaminio, Rum. 1:6-17.
3
2. Halipo kanisa kongwe au kanisa jipya lililopandwa ambalo likikataa kufanya kazi bila kuchoka katika kueneza Injili litakuwa na nguvu au afya.
U T U M E K A T I K A M I J I
3. Kudhihirisha nguvu za Roho pamoja na kutangaza Neno la Mungu ni muhimu kwa ufanisi wa kufanya wanafunzi katika jamii za mijini.
a. Ishara na ajabu za Roho Mtakatifu, Rum. 15:18-20 – “Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, 19 kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kando kando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu; 20 kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine.”
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker