Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | MKAZO KUHUSU UZAZ I : UKUA J I WA KAN I SA / 435

katikati hata ya jumuiya ndogo ya Wakristo wanaopaswa kukamilisha kazi ya Mungu katika jumuiya yao.

10. Fikiria kujizalisha (2 Tim. 2:2; Flp. 1:18). Katika kila shughuli na mradi unaoanzisha, fikiria jinsi ya kuwaandaa wengine kufanya kile unachokifanya kwa kudumisha uwazi kuhusu njia na malengo ya jitihada zako za kimishenari.

V. Neno la Mwisho: Njia ya haraka zaidi, yenye tija zaidi na ya kibiblia ya uinjilisti na ufuasi ulimwenguni ni kupanda makanisa katika tamaduni mbalimbali!

Hitimisho • Kupanda makanisa kama utii kwa Agizo Kuu la Kristo kunahusisha hatua tatu za msingi: Kuinjilisha, Kufuasa na Kuwezesha. • Tunapofanya uinjilisti kwa waliopotea, tunawashirikisha Habari Njema wale ambao hawajasikia kazi ya Mungu ya wokovu katika Yesu. • Tunawafuasa wanafunzi wapya kuishi maisha ya Kikristo kwa kuweka msingi kwa ajili ya jumuiya imara ya Kikristo kwa faida ya miaka mingi ijayo. • Tunawawezesha viongozi na kanisa kwa ajili ya kujitegemea, tukiwasaidia kujizalisha wenyewe huku wakishirikiana na makanisa mengine yenye nia moja nao. Maswali yafuatayo yalikusudiwa kukusaidia kupitia maudhui ya video. Agizo Kuu la Bwana Yesu linamaanisha kwamba tumeitwa kwenda kwa mataifa yote tukifanya wanafunzi kwa jina lake. Tunatimiza Agizo Kuu tunapopanda makanisa yenye afya na uwezo wa kujiendesha miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu duniani. Tunatekeleza hili kupitia Kuinjilisha, Kufuasa na Kuwezesha . Uwezo wako wa kuelewa na kutumia kanuni hizi unaweza kuwa ndilo jambo la tofauti katika kuhudumu kwa ufanisi katikati ya jamii maskini za mijini, kwa hiyo uwezo wako wa kuzielewa na kuzifafanua ni muhimu. Jibu maswali yafuatayo kwa ukamilifu, na mara zote tumia Maandiko kama msingi wa mawazo yako.

3

U T U M E K A T I K A M I J I

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker