Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
436 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
1. Kwa nini inaweza kusemwa kwamba uinjilisti ndio kitovu cha umisheni na uenezi wote wa Kikristo? Kwa nini kudhihirisha tu Injili katika matendo mema peke yake hakutoshi katika huduma ya Ufalme? 2. Je, ishara na maajabu ya Roho Mtakatifu vilikuwa na nafasi gani katika huduma ya mitume katika kushuhudia neema ya Mungu? Je, vinaweza au vinapaswa kuwa na nafasi gani katika kazi yetu leo mijini? 3. Je! ni Injili gani hasa tunayoitwa kuitangaza katika huduma yetu? Ni kwa namna gani somo lako lilimeweza kuweka muhtasari wa mchakato wa upandaji wa kanisa kupitia vipengele muhimu vya mchakato huo? Tafadhali, taja vipengele husika vya mchakato wa kupanda kanisa. 4. Katika hatua ya Uinjilishaji, toa tafsiri ya hatua ya «Jiandae» ya kupanda kanisa. Sambamba na hilo, toa tafsiri ya hatua ya «Anza» katika mchakato wa upandaji kanisa. Mambo gani yanahusika katika kila moja ya hatua hizo, na ni aina gani za shughuli zinazohusiana na kila moja ya hatua hizo? 5. Kwa nini kufuasa Wakristo wapya katika imani ni hatua muhimu sana katika kufanya wanafunzi wa kweli? Je, kanisa la mahali pamoja lina nafasi gani katika kumfundisha mwongofu mpya habari za Kristo? Je, funguo za kuwafuasa waamini kuishi maisha ya Kikristo ni zipi? 6. Elezea awamu za «Kukusanya» na «Kulea» za upandaji kanisa katika huduma za mijini, na uhusianishe jinsi awamu hizi zinavyotuwezesha Kufuasa waamini wapya kukua katika Kristo. Je, zinafanana kwa njia gani, zinatofautiana kwa njia gani, na ni nini kinachohusika katika kila moja? 7. Kwa nini ni muhimu kwa makanisa kutafuta mara kwa mara kujizalisha yenyewe kupitia uinjilisti endelevu na kufuasa wengine? Kuna uhusiano gani kati ya afya ya kiroho na tunda la roho? 8. Eleza awamu ya «Mpito» ya Uwezeshaji . Je, ni kwa namna gani uwezeshaji katika uhalisia wake ni «uwekezaji» katika uongozi na ushirika wa kanisa jipya? 9. Katika awamu ya “Mpito” ya upandaji kanisa, taja sifa tatu za kanisa la kienyeji lililokomaa kiasi cha kujiendesha pasipo msaada wa wamishenari waanzilishi. Elezea kwa ufupi kielelezo cha Hesselgrave cha upandaji makanisa katika tamaduni mchanganyiko. Kuna uhusiano gani kati ya uelewa wa sifa tatu za kanisa la kienyeji linalojiendesha katika kielelezo cha Hesselgrave, na vipengele vikuu vitatu vya upandaji kanisa (Kuinjilisha, Kufuasa na Kuwezesha)?
3
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker