Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | MKAZO KUHUSU UZAZ I : UKUA J I WA KAN I SA / 437

10. Fanya muhtasari wa kanuni kumi za upandaji kanisa katika tamaduni mbalimbali. Je, unakubaliana na kauli kwamba “Njia ya haraka zaidi, yenye tija zaidi na ya kibiblia ya uinjilisti na ufuasi ulimwenguni ni kupanda makanisa katika tamaduni mbalimbali”? Elezea jibu lako.

UHUSIANISHAJI

Somo hili linalenga katika kukupa muhtasari wa jumla wa theolojia, mbinu, na mtazamo muhimu katika kufanya huduma yenye ufanisi katika miji. Ili tuwe na matokeo zaidi katika kueneza Ufalme wa Mungu katika miji, sisi kama watumishi wake tulioitwa lazima tuwe na ulewa makini na sahihi wa kile ambacho Mungu anafanya ulimwenguni kupitia kuhubiriwa kwa Injili. Baba amemwinua Yesu na kumketisha mkono wake wa kuume kama Bwana na Mwokozi, na sasa, kwa njia ya Roho Matakatifu, Injili inatangazwa duniani kote. Tunapopanda makanisa ya Yesu Kristo yenye afya na nguvu mijini kupitia uinjilisti, kufuasa na kuwezesha tunaweza kuona wanaume na wanawake, wavulana na wasichana wakiongoka, kukua na kuwa mashahidi wa Ufalme wa Kristo wenye kuzaa matunda mahali wanapoishi, katika maeneo yao ya michezo na burudani, na makazini kwao. • Katika kila hatua na nyanja ya umisheni, mafundisho, mahubiri, na uenezi, ni lazima tumsihi Bwana wetu Yesu kwa ajili ya kupata msaada na mwongozo, kwa sababu yeye peke yake ndiye anayeweza kutuwezesha kuvuna roho na kupanda makanisa katika majiji. • Agizo Kuu la Kristo ni wito wa kwenda kufanya mataifa kuwa wanafunzi, na ufuasi huu wa kina hauwezi kuzalishwa na kuthibitishwa kuwa halali nje na jumuiya ya Kikristo. • Mkakati mzuri wa upandaji kanisa unaweza kufupishwa katika awamu vifuatavyo: kujiandaa, kuanza, kukusanyika, kulea, na mpito. Awamu hizi zimejumuishwa katika hatua tatu zilizounganishwa: kuinjilisha waliopotea, kufuasa wanafunzi wapya kuishi maisha ya Kikristo, na kuwawezesha viongozi na kusanyiko kujizalisha na kushirikiana na makanisa mengine yenye nia moja. • Kanuni za upandaji kanisa katika tamaduni mchanganyiko zinatoa msingi bora na imara kwa juhudi zetu za kuhudumu miongoni mwa maskini mijini. Zikiwa zimechukuliwa kutoka kwenye uzoefu wa mitume ulioainishwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, kanuni hizi zimeweka wazi ufahamu muhimu wa huduma za mijini zenye matokeo. Zinahusisha kuthibitisha kwamba Yesu ni Bwana, changamoto ya kuinjilisha, kufuasa, na kuwawezesha watu

Muhtasari wa Dhana Muhimu Ukurasa wa 186  5

3

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker