Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

438 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

ambao hawajafikiwa ili kufikia watu wengine, na hitaji la kujumuisha watu wote, kutoegemea upande wowote kitamaduni, na kuvuka vizuizi vya utaifa, matabaka, jinsia na lugha ili kuiweka wazi Injili ya Ufalme kwa wale tunaotafuta kuwafikia.

Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu ukuaji wa kanisa na uzazi. Ili kukabiliana na dhana hizi, lazima tutafute asili jumuishi ya huduma ya mijini yenye ufanisi. Tunahubiri injili kwa nia ya kuwafuasa waamini wapya katika imani, na kuwaandaa kwa dhamira ya kuwawezesha Wakristo hawa wanaokua kuwashirikisha watu wengine imani yao. Unapotafakari juu ya hatua hizi na mawazo haya, ni maswali gani mahususi ambayo yamekuja akilini? Fikiria maswali yako mwenyewe, unapojibu maswali yaliyopo hapa chini. • Kwa nini fundisho kuhusu ubwana wa Kristo ni la msingi sana kwa mtazamo wowote halali wa huduma au uenezi wa Injili? Je, upi ni uelewa na matumizi yako ya fundisho hili muhimu katika maisha yako leo? Elezea. • Je, umesikia wito kutoka kwa Bwana wa kuwa mhudumu wa Injili? Ni kwa jinsi na kwa njia gani? Ikiwa umesikia wito kama huo, ni lini hasa ulitambua kwa mara ya kwanza kwamba amekuita kwenye huduma hiyo? • Je, unawezaje kuuelezea uwezo wako wa kutumaini ubwana wa Kristo wakati wa magumu, mateso, na shida? Je, wewe ni mwenye hofu, yaani, unahangaika juu ya maeneo mbalimbali za maisha na huduma yako? Ni kwa jinsi gani matumizi ya fundisho la Kristo yanaweza kukusaidia kushinda woga na mahangaiko yako katika maeneo haya? • Kipi kuhusu mchakato wa upandaji kanisa kinaonekana kuwa wazi zaidi kwako? Ni kipi katika mchakato huo hakiko wa zaidi? Je, umewahi kufikiria uwezekano wa Mungu kukutaka ushiriki katika kuanzisha makanisa mapya kwa ajili yake? Kwa nini ndiyo au kwa nini sio? • Jadili ukweli na uhalali wa kibiblia wa kauli ifuatayo: “Njia ya haraka zaidi, yenye tija zaidi na ya kibiblia ya uinjilisti na ufuasi ulimwenguni ni kupanda makanisa katika tamaduni mbalimbali.” Je, unakubaliana na kauli hii? Kwa nini ndiyo au kwa nini sio? • Kati ya maeneo matatu mapana ya huduma ya mjini ( Kuinjilisha, Kufuasa, na Kuwezesha ), ni eneo lipi unahisi kuvutiwa nalo zaidi na umekirimiwa uwezo na kipawa kwa ajili ya kulifanya? Je, wewe ni sehemu ya kusanyiko

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi Ukurasa wa 186  6

3

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker