Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
440 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
kinachoweza kufanywa au kuamuliwa kanisani bila wao kuhusika na kuidhinisha. Wengine wanadokeza kwamba hii inaenda kinyume na mafundisho ya Biblia juu ya ubwana wa Yesu, ambaye ndiye kiongozi mkuu wa kweli na wa pekee wa Kanisa. Kama kanisa llingekuomba utoe fundisho juu ya hili, ungewashauri kutumiaje fundisho la ubwana wa Yesu katika hali yao? Tuanzishe Ibada YetuWenyewe Katika kanisa fulani la mjini dogo lakini linalokua, vijana wamechoshwa kabisa na ibada za kimapokeo za ushirika huo. Ingawa mafundisho ya mchungaji ni mapya na yanajenga, na waamini kanisani wana upendo na kujali, mitindo inayokumbatiwa katika ibada ni ya kitamaduni na ya kizamani kiasi kwamba wengi wa vijana wanaokuja kanisani wanahisi kuachwa na kutengwa. Mchungaji, akizingatia uhuru wetu katika Kristo, anataka vijana waanzishe ibada yao wenyewe. Hoja yake ni ya wazi: “Kwa kuwa Injili inaweza kushinda kizuizi chochote cha utamaduni au tabaka au ukabila, hakuna sababu ya kwa nini hatuwezi kushinda vizuizi vya desturi, muziki, na utamaduni pia.” Badhi wanafikiri aina hii ya mafundisho itapelekea katika uchakachuzi wa Injili, na hivi karibuni timu ya uongozi itaanza kujadili uwezekano huo. Ungeshauri timu ya uongozi kushughulikia vipi suala hili kanisani? Hisani Huanzia Nyumbani Mchungaji kiongozi wa kanisa fulani amekuwa katika majadiliano endelevu na viongozi wa kanisa hilo kuhusu pendekezo jipya ambalo limezua mjadala mkubwa ndani ya kanisa. Badala ya kuhamia jengo kubwa zaidi nje ya “mtaa yenye uhitaji” ambamo kanisa limekuwa kwa miaka kumi iliyopita, mchungaji anataka kubaki. Pendekezo lake si kwenda kwenye jengo kubwa zaidi, bali kuwaandaa washirika wa kanisa kwenda kupanda kanisa lingine katika mtaa huo huo. Mchungaji, akielezea uwezo kuwaleta wanafunzi wapya kwa Kristo kuptia upandaji kanisa, anathibitisha imani yake kwamba hakuna njia iliyo ya kibiblia au ya haraka zaidi. Wale walio upande mwingine, huku wakiwa hawakatai upandaji kanisa, wanataka kuwa na kanisa moja lenye nguvu, ambalo linaweza kuwa na uwezo bora wa kupanda makanisa mapya ikiwa “kanisa mama” litakuwa na nguvu. Baada ya yote, wanasema, hisani inapaswa kuanza nyumbani. Kama ungekuwa mchungaji mshiriki wa kanisa, ungetafutaje kusuluhisha mzozo huu kuhusu mbinu?
3
3
U T U M E K A T I K A M I J I
4
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker