Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | MKAZO KUHUSU UZAZ I : UKUA J I WA KAN I SA / 441

Wazo la msingi zaidi la kitheolojia ambalo linaweka msingi wa uelewa wetu wote wa uinjilisti, ufuasi, na upandaji kanisa mjini ni ubwana wa Yesu Kristo. Kwa sababu Yesu ameinuliwa na kuketishwa mkono wa kuume wa Baba akiwa Bwana mfufuka na Masihi mpakwa-mafuta, sasa ana nafasi ya kichwa juu ya vitu vyote, si kwa Kanisa tu bali pia katika kuenea kwa Ufalme ulimwenguni, akiwa Bwana wa mavuno. Kila nyanja ya huduma iko chini ya uongozi na uwezo wake. Agizo Kuu la Kristo ni wito wa kwenda kufanya mataifa kuwa wanafunzi, na ufuasi huu wa kina hauwezi kuzalishwa na kuthibitishwa kuwa halali nje na jumuiya ya Kikristo. Mkakati mzuri wa upandaji kanisa unaweza kufupishwa katika awamu vifuatavyo: kujiandaa, kuanza, kukusanyika, kulea, na mpito. Hatua tatu huunganisha awamu hizi: kuinjilisha waliopotea, kufuasa wanafunzi wapya kuishi maisha ya Kikristo katika Kanisa, na kuwawezesha viongozi na kusanyiko kujizalisha na kushirikiana na makanisa mengine yenye nia kama hiyo. Hekima ya kanuni zinazotokana na uzoefu wa mitume unaotajwa katika kitabu cha Matendo hutupatia maarifa muhimu kwa ajili ya huduma ya mijini yenye matokeo. Zinahusisha kuthibitisha kwamba Yesu ni Bwana, changamoto ya kuinjilisha, kufuasa, na kuwawezesha watu ambao hawajafikiwa ili kufikia watu wengine, na hitaji la kujumuisha watu wote, kutoegemea upande wa kitamaduni, na kuvuka vizuizi vya ukabila, matabaka, jinsia na lugha ili kuiweka wazi Injili ya Ufalme kwa wale tunaotafuta kuwafikia. Kama ungependelea kufuatilia baadhi ya mawazo ya Ukuaji wa Kanisa – Kuongezeka katika Idadi na Ubora , unaweza kujaribu vitabu hivi: Ellul, Jacques. The Presence of the Kingdom . New York: Seabury Press, 1967. Garrison, David. Church Planting Movements . Bangalore, India: WIGTake Resources, 2004. Hopler, Thom. A World of Difference . Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1981. Pippert, Rebecca Manley. Out of the Saltshaker and Into the World . Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1979.

Marudio ya Tasnifu ya Somo Ukurasa wa 188  8

3

U T U M E K A T I K A M I J I

Nyenzo na Bibliografia

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker