Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

442 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Sasa ni wakati wako wa kuweka maana za maarifa haya ya kifundisho na kitheolojia katika hali yako binafsi ya maisha na vilevile kuzihusianisha na kivitendo na huduma yako halisi. Fikiria kwa msingi wa kile unachotaka kutafakari, kuzingatia upya, na kuombea katika wiki hii yote ijayo. Ni nini kinaonekana kuchochewa hasa na Roho Mtakatifu ndani yako kama matokeo ya kutafakari kwako, kujifunza, na majadiliano juu ya asili ya ubwana wa Kristo, Agizo Kuu la kwenda kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi, na mchango wako mwenyewe kwa hayo? Je, ni kwa njia gani unahisi kuitwa kuchangia leo hii katika wito wa kufanya wanafunzi wa Yesu, kwenye familia yako, kanisani kwako, mtaani, au kazini? Je, unahisi wito rasmi zaidi wa huduma ya Injili katika maisha yako, kwa maneno mengine, Mungu anakuita au amekuita kuifanya huduma kuwa kazi yako ya wakati wote? Je, unaweza kumshirikisha nani shauku na mzigo huu? Umefanya nini hasa hadi sasa kuhusiana na mzigo wako kwa mchungaji wako na viongozi wa kiroho, kwa mume au mke wako, kwa marafiki na jamaa zako? Je, wewe binafsi unawezaje kutoa muda, talanta, au hazina kwa ajili ya kazi ya upandaji makanisa, katika jamii yako, kupitia kanisa lako, au hata nchi za ng’ambo? Je, Mungu anakuita ufikirie mabadiliko katika kazi yako, ratiba yako au mwelekeo wako wa maisha ili kutafuta kitu kinacholingana na kuendana zaidi na kueneza Injili kwa waliopotea? Kama Mungu hakuelekezi katika aina hizi za mabadiliko, unawezaje kutumia mafundisho haya maishani mwako ili uweze kuwa mwenye ufanisi zaidi katika kufanya wanafunzi wa Bwana Yesu? Je, Roho Mtakatifu anaweka hali fulani akilini mwako kuhusu namna unavyoweza kutumia mafundisho haya katika maisha yako leo? Tafakari katika hali ya maombi kuhusu maswali haya na yanayohusiana nayo, na umwombe Roho aweke wazi namna anavyokupa changamoto ili uweze kuzitafakari na kuzipa mwitikio wako kuhusiana na mada hii katika somo hili. Tunapotafuta sehemu yetu katika kazi hii kuu ya kutimiza Agizo Kuu, itakuwa muhimu kwetu kuwa waombaji, hata kujizoeza nidhamu ya kufunga na kutafakari ili kumpa Mungu nafasi ya kusema na mioyo yetu kwa uwazi zaidi. Hakikisha kwamba unamwomba mshauri wako na wafanyakazi wenzako kuomba kwa ajili ya uongozi na mwelekeo maalum katika maisha yako unapotafuta zaidi na zaidi njia za vitendo ambazo unaweza kujiunga na jitihada hii kuu ya kumfanya Yesu ajulikane katika maeneo yote ambayo bado hazijasikia habari za neema yake ya upendo na Ufalme ujao. Tenga muda wa kumwomba Bwana kimaalum kwa ajili ya mwongozo na hekima unapofuatilia wito wako chini ya ubwana wa Kristo ili kueneza Ufalme wake katika

Kuhusianisha Somo na Huduma

3

U T U M E K A T I K A M I J I

Ushauri na Maombi Ukurasa wa 189  9

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker