Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

446 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. 13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. 15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. 16 Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni. Je, tuna wajibu gani hasa kwa ajili ya ustawi wa wengine, wawe ni marafiki, familia, majirani, wageni au jamaa, maadui au wapendwa? Inaonekana kwamba ndani yetu sote kuna tabia ya kuwapenda wale tu walio wa «karibu,» watu wale tunaowahesabu kuwa marafiki, au ndugu wa karibu. Kwa nini tunapaswa kudhabihu rasilimali na fursa zetu chache za thamani kwa niaba ya watu ambao ama hatuwajui vizuri, kwa wale ambao wana tabia ya kutumia vibaya wema wetu, au mbaya zaidi, kwa wale ambao wanatuchukia kabisa? Mwisho wa yote, jirani ambaye tumeitwa kumpenda kama tunavyojipenda sisi wenyewe ni yupi? (taz. Law. 19:18). Mwanzo 4 ina moja ya matukio makuu lakini ya kutisha katika Maandiko yote. Likiwa limetokea baada ya Anguko kuu la uchungu wa kwanza wa mwanadamu ambapo uasi wake wa hiari ulipelekea laana na kifo, tunaona dhahiri moja ya matokeo yake. Matengano, Wivu, Chuki na uovu, ambavyo vinasababisha mauaji ya kikatili na kujihesabia haki. Ingawa kwa juu juu hadithi hii inaonekana ikiuhusu mgogoro kati ya ndugu wawili, tukiangalia kwa karibu tunaona maana kubwa zaidi. Katika hadithi hii ya mgogoro kati ya Kaini na Habili ama kwa hakika unabii wa Mwanzo 3:15 unatimizwa kwa uthabiti: uzao wa mwanamke unakutana na uzao wa nyoka. Kaini anaufungulia uovu unaomnyemelea mlangoni, anamuua kikatili ndugu yake mwenyewe kwa sababu ya wivu na uovu, analaaniwa, na anakuwa mwanzilishi wa kwanza wa mji na jamii isiyomcha Mungu. Namna hii ya kukataa mapenzi ya Mungu, ya kuwachukia wale ambao kwa hakika wanayashika mapenzi ya Mungu, inatajwa katika Agano Jipya kama “njia ya Kaini” (Yuda 11), au “dhambi dhidi ya ndugu ya mtu” (1 Yoh. 3:12, 15). Kwa ujumla, hadithi hii inafichua aina ya ukosefu wa tumaini na utii kwa Bwana ambao husababisha wivu hatari kwa watu wa Mungu mwenyewe. Wivu huu ni wa kuua, na hupelekea kwenye vurugu, mauaji, matengano, na hatimaye kwenye hukumu ya Mungu mwenyewe. Katika andiko hili, ndugu wawili, Kaini na Habili wametofautishwa, na kila mmoja kusimamishwa dhidi ya mwingine, huku kifungu

4

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker