Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | KUT ENDA HAK I NA KUPENDA REHEMA : HAK I NA I SHUKE / 447
kizima hapo juu kikiwatofautisha kwa kila namna. Kaini anaonyeshwa kama mtu ambaye kazi yake, kama mfafanuzi mmoja asemavyo, «inamfungamanisha na laana,» mtu anayeilima ardhi, (taz. Mwa. 4:2; taz. 3:17). Habili, kwa upande mwingine, anatokea kama mchungaji wa kondoo, anayemwabudu Mungu kupitia dhabihu za mifugo yake, namna ya ibada ambayo ni kivuli cha dhabihu kuu ya Bwana wetu Yesu Kristo. Kulingana na Mtume Yohana, tendo la Habili la kutoa dhabihu katika ibada lilikuwa la haki, wakati matendo ya Kaini yalikuwa maovu (1 Yoh. 3:12). Tunajua kwamba kiini cha dhabihu kilikuwa ni utoaji wa sadaka kwa imani, ambayo bila hiyo haiwezekani kumpendeza Mungu (Ebr. 11:6). Badala ya kujifunza aina ya dhabihu ambayo ingempendeza Mungu, ukosefu wa tumaini kwa Mungu ambao Kaini alikuwa nao unaonyeshwa katika mwitikio wake kwa tendo la Mungu kukataa matoleo ya mazao yake. Kaini alikasirika, hata akakataa kusikiliza ushauri wa Mungu mwenyewe (4:6-7). Ushauri wa Mungu ulikuwa dhahiri: kwa kweli, kama Kaini angefanya lililo sawa na hivyo kumpendeza Mungu, hali yake ingekuwa vizuri. Hata hivyo, dhambi ilikuwa inamnyemelea kama mnyama mkali aliye tayari kumshinda ikiwa angekataa ushauri huo na kukubali uovu katika kuvunjika kwake moyo. Dhambi ilimtamani lakini angeweza kuishinda. Kaini alikataa ushauri mwema wa Mungu na kumuua ndugu yake. Badala ya kukiri kosa, yeye alikana wajibu wake kwa ndugu yake. “Je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” Hapa kuna taswira ya wazi ya moyo uliokufa na wenye giza, ambao unaweza kumfanya mtu kumchukia ndugu yake kiasi kwamba akakataa wajibu wowote kwa ajili ya ustawi wake, na hata kumuua, na kutojutia. Hapa, ndipo penye tatizo la kisasa – kwamba uasi dhidi ya Mungu hujenga utengano usioepukika na ndugu zetu, na ikiwa hautadhibitiwa, mwishowe unaweza kusababisha mauaji na laana. Mungu ni mwenye neema hata katika hukumu, akimlinda Kaini katika kumfukuza kwake, kwa alama au ishara ambayo ingewazuia wale wanaotaka kulipiza kisasi kwa ajili ya mauaji ya Habili. Hata katika hili, Kaini mwasi anakaidi adhabu ya Mungu ya kutangatanga na badala yake anajenga mji wa kwanza katika nchi ya Nodi (maana yake «kutangatanga»), mashariki mwa Edeni (ms. 16). Tunapoanza somo letu, mambo ya kujifunza yapo wazi kabisa. Mahusiano yetu na Mungu na mahusiano yetu na watu wengine yameunganishwa kwa kina; hakuna anayeweza kudai kutembea kwa kina na Mungu na akamchukia ndugu yake (1 Yoh. 4:20-21), na ikiwa tunampenda Mungu, tutajitoa kwa niaba ya kaka na dada zetu (1 Yoh. 3:14-). Kwa hakika sisi ni walinzi wa kaka na dada zetu, tulioitwa kutunzana, na sio kulana sisi kwa sisi katika kujilinganisha kwetu, wivu, chuki, na jeuri. Kuwa karibu na Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ni kuwajali wengine kwa kina, kwa maana Mungu ni pendo. Yule anayedai kumjua Mungu na hana upendo, hamjui Mungu hata kidogo (1 Yoh. 4:7-8).
4
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker