Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

448 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Kwa sisi tunaomtumikia Kristo mjini ni lazima tuushikilie ukweli huu kwa mioyo yetu yote. Mwenendo muhimu, unaokua, na wa kina pamoja na Mungu utajidhihirisha kila mara katika matendo fulani maalum na thabiti ya upendo na rehema kwa kaka na dada zetu, majirani zetu, na hata adui zetu. Je, sisi ni walinzi wa ndugu zetu? Hakika, ni kweli, ikiwa tu tumekombolewa kwa damu ya Yesu Kristo. Sikiliza ufafanuzi wa Mtume Yohana kuhusu Kaini na Habili: 1 John 3.11-15 – Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi; 12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki. 13 Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia. 14 Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti. 15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake. Na tuikubali amri mpya ya Bwana wetu ya kupendana. Hakika sisi ni walinzi wa ndugu zetu. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu Mtakatifu, unaishangaza hekima ya ulimwengu katika kutoa ufalme wako kwa wanyenyekevu na wenye moyo safi. Utupe njaa na kiu ya haki na ustahimilivu katika kuipigania amani, ili kwa maneno na matendo yetu ulimwengu upate kuona ahadi ya ufalme wako, iliyofunuliwa katika Yesu Kristo Bwana wetu, anayeishi na kutawala pamoja nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele na milele. Amina.

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

4

U T U M E K A T I K A M I J I

~ Presbyterian Church (U.S.A.) na Cumberland Presbyterian Church. The Theology and Worship Ministry Unit. Book of Common Worship . Louisville, Ky.: Westminister/John Knox Press, 1993. uk. 209.

Pitia upya na mwenzako, andika na/au jikumbushe kifungu cha mstari wa kumbukumbu uliopewa kwenye kipindi cha darasa lililopita: Waefeso 6:10-13.

Mapitio ya Kukariri Maandiko

Wasilisha muhtasari wako wa kazi ya kusoma ya juma lililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache ya mambo makuu ambayo waandishi walikuwa wakitafuta kuyaainisha katika kazi ya usomaji uliyopewa (Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukusanya

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker