Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | KUT ENDA HAK I NA KUPENDA REHEMA : HAK I NA I SHUKE / 449

KUJENGA DARAJA

Mara Zote, Familia Kwanza! Katika mjadala wakati wa darasa la Shule ya Jumapili ya watu wazima, wanafunzi kadhaa wanajadili “mpangilio wa upendo” ambao Mkristo ameitwa kuwa nao. Je, tunapaswa kuzipenda ndoa zetu na wanafamilia kwanza, katika namna ambayo ni ya tofauti, kabla na kwa namna bora zaidi kuliko upendo mwingine tulionao. Baadhi wanasisitiza kwamba amri ya upendo inadokeza kuwa tunapaswa kuwapenda watu wote kwa kujidhabihu, hata adui zetu. Wengine wanasoma andiko ili kudokeza kwamba tunapaswa kuwatendea watu wote mema, lakini hasa kwa washirika wa nyumba ya Mungu (taz. Gal. 6:10). Je, upi ni uelewa wako kuhusu mipangilio wa viapaumbele mbalimbali vya upendo ambavyo mwanafunzi wa Yesu anaitwa kudhihirisha kwa wengine? Je, tunapaswa kuwapenda watu tofauti tofauti kwa viwango tofauti tofauti, au tumeitwa kumpenda kila mtu katika namna sawa? Imani ya Ubinadamu ni Mbaya! Mwishoni mwa karne ya ishirini wasomi kadhaa wa Kikristo walianza kujadili wazo la imani ya ubinadamu (humanism) katika Ukristo, wazo kwamba wanadamu wote wameumbwa kwa sura ya Mungu na kwa hiyo wanastahili haki za msingi za kibinadamu ambazo ni lazima kuzilinda na kuzitetea. Wakati ambapo baadhi ya viongozi wa Kikristo wa kiinjili walikubali mtazamo huu, wengine wengi walikataa wakiuona kama uchakachuzi na hatua ya kwanza kuelekea kwenye falsafa ya kilimwengu ( universalism ). Walijenga hoja yao kwa msingi kwa watu wanaotetea hoja ya ubinadamu wanajenga mawazo na maelezo yao kwamba uhai wa mwanadamu ndio uumbaji wa juu zaidi kuliko uumbaji wote, kana kwamba ndio mwisho wa vitu vyote. Pasipo shaka yoyote, huu sio msimamo wa Kikristo; Mungu mweza yote, kusudi lake kuu na mapenzi yake, ndio mwisho wa mambo yote. Kwa upande mwingine, Wakristo wanaotetea hoja ya ubinadamu wanatoa utetezi wao kwamba wokovu unathibitisha upekee na uajabu wa maisha ya mwanadamu kwa Mungu; alimtoa Mwana wake wa pekee ili kukomboa uumbaji wake, hasa wanadamu. Una maoni gani kuhusu uhalali wa dhana ya humanism katika Ukristo? Je, kweli inawezekana kuwa Mkristo na wakati huo huo mwenye msimamo wa humanism ? Uhai wa Mwanadamu Umeanza na Uumbaji, sio Anguko Wengi wanaulalamikia ukweli kwamba idadi ya theolojia kadhaa za Kiprotestanti juu ya maisha ya mwanadamu inaonekana kuweka msisitizo wake wote juu ya Anguko, tukio la kutisha la uasi wa kimakusudi dhidi ya mapenzi ya Mungu uliofanywa na Adamu na Hawa ambao uliuingiza uumbaji katika laana na machafuko. Hata

1

Ukurasa wa 195  4

2

4

U T U M E K A T I K A M I J I

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker