Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
450 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
hivyo, kauli za kwanza kuhusu mwanadamu hazianzi na Anguko, bali na uumbaji, ambapo Mungu alimfanya mwanadamu kwa mfano wake mwenyewe, mtu mzuri, mbunifu, na huru. Je, inaleta tofauti gani ikiwa utaegemeza fikira zako za msingi kuhusu wanadamu kwenye tukio la uumbaji badala ya anguko la mwanadamu? Je, katika mijadala yetu ya kitheolojia, ni kwa jinsi gani tunapaswa kuelewa umuhimu wa mambo haya yote mawili ya msingi tunapoelezea asili na kusudi la mwanadamu katika ulimwengu?
Haki na Ishuke: Maono na Theolojia ya Ufalme Sura ya Mungu kama Msingi wa Masuala na Matendo ya Kijamii
Mch. Dk. Don L. Davis
MAUDHUI
Msingi wa kutenda haki na kupenda rehema miongoni mwa maskini mjini ni uthibitisho wa imago Dei katika kila mvulana, msichana, mwanamke, na mwanamume. Kila mtu anastahili kutunzwa kwa sababu anashiriki katika imago Dei isiyo na kifani, ya kipekee, na isiyo na mbadala. Kwa sababu wote wameumbwa kwa sura ya Mungu, wanadamu wote ni wa pekee na wenye thamani. Taswira hii hujumuisha sababu za kwa nini tunapaswa kutenda haki na kupenda rehema miongoni mwa watu binafsi, familia, makabila, na mataifa yote duniani. Kila mmoja wao kama abebaye imago Dei atachukuliwa kuwa wa thamani na asiye na mbadala. Lengo letu katika somo hili, Sura ya Mungu kama Msingi wa Masuala na Matendo ya Kijamii , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Ufafanuzi mzuri wa imago Dei (yaani, sura ya Mungu) katika Maandiko, ni “Hali ya upekee wa wanadamu wote kwamba wameumbwa kama Mungu na kwa hivyo wanastahili heshima, ulinzi, na utunzaji wetu.” • Uthibitisho wa mwanadamu kuumbwa kwa mfano wa Mungu ni uthibitisho wa kipekee, hakuna kiumbe mwingine au malaika anayesemekana kuumbwa kwa mfano wa Mungu. • Ingawa namna mahususi ambayo wanadamu wameumbwa kwa mfano wa Mungu haijasemwa waziwazi katika Maandiko, kuna uthibitisho unaoonyesha kwamba wanadamu wanashiriki sifa zinazolingana na za nafsi ya Mungu mwenyewe, yaani, haiba yetu, ufahamu wetu, uwezo wetu wa kuchagua, na uwezo wetu wa kimaadili. • Ukweli kwamba wanadamu waliumbwa katika imago Dei unadokeza kwamba wanadamu wote wanashiriki sura hii;
Muhtasari Ukurasa wa 195 5
4
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker