Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
454 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
b. Ufahamu wetu : tunafanana na Mungu katika kujitambua na ufahamu.
c. Hiari na Utashi wetu : tunafanana na Mungu katika uwezo wa kuchagua.
d. Uwezo wetu wa kimaadili : tunafanana na Mungu katika hali ya maadili.
D. Thamani ya wanadamu: wanadamu wote wanashiriki imago Dei .
1. Wanadamu wote wanashiriki sura hii: hakuna tofauti miongoni mwa wanadamu kuhusu sura ya Mungu, Mdo. 17:26.
2. Sura hii ni msingi wa kuelewa uhusiano wa Mungu na wanadamu, na mwitikio wa wanadamu baina yao, Yak. 3:9.
3. Sisi ni wabaya kwa sababu ya laana, lakini wanadamu ni wa pekee na wa thamani, kwa sababu ya uumbaji.
4
U T U M E K A T I K A M I J I
II. Umuhimu wa Imago Dei katikaWanadamu: Uumbwaji wa Ajabu waWanadamu
A. Wanadamu wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Mwa. 1:26-28 – Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker