Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

456 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

6. Maana yake: Wanadamu wote, bila kujali historia au tabia zao, wameumbwa chini kidogo kuliko malaika ; Mungu amewavika taji la utukufu, heshima, na utawala .

C. Wanadamu wameumbwa kwa jinsi ya ajabu na ya kutisha. Zab. 139:13-16 – Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu. 14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, 15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; 16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.

1. Ameumbwa kwa uwezo mkuu wa kiakili wa Mwenyezi Mungu katika namna zote (namna ya kimwili na ya kiroho).

2. Ameumbwa kwa ufundi na utunzaji maalum wa Mungu.

3. Tangu utotoni hadi kufa: Ubunifu wa kibinafsi wa Mungu upo kwenye maisha ya kila mwanadamu.

4

U T U M E K A T I K A M I J I

4. Ukuu wa Mungu unagusa na kuathiri siku za kila mwanadamu.

5. Maana yake: Kila mwanadamu ni zao la fikra kuu kabisa ya Mungu na kazi yake, akiwa ameumbwa naye kwa jinsi ya ajabu na ya kutisha kama kiumbe wa kipekee na wa thamani isiyo na kikomo .

D. Maisha ya mwanadamu yanalishwa katika utele na kuruzukiwa na Mungu.

Zab. 104:13-24 – Huinywesha milima toka orofa zake; Nchi imeshiba mazao ya kazi zako. 14 Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi, 15 Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung’aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker