Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | KUT ENDA HAK I NA KUPENDA REHEMA : HAK I NA I SHUKE / 457

mtu moyo wake. 16 Miti ya Bwana nayo imeshiba, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. 17 Ndimo ndege wafanyamo vitundu vyao, Na korongo, misunobari ni nyumba yake. 18 Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, Na magenge ni kimbilio la wibari. 19 Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, Jua latambua kuchwa kwake. 20 Wewe hufanya giza, kukawa usiku, Ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu. 21 Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo, Ili kutafuta chakula chao kwa Mungu. 22 Jua lachomoza, wanakwenda zao, Na kujilaza mapangoni mwao. 23 Mwanadamu atoka kwenda zake kazini, Na kwenye utumishi wake mpaka jioni. 24 Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako.

1. Utele katika dunia umetolewa kwa utunzaji wa ukarimu wa Mungu.

2. Mungu ndiye chanzo cha kila zawadi nzuri na kamilifu inayofurahiwa na wanadamu kila mahali, Yak. 1:17.

3. Dunia na kila kilichomo ndani yake vimeruzukiwa kwa mikono ya Mungu kwa ajili ya viumbe vyote vikaavyo duniani.

4

4. Nchi ni ya Bwana, na imejaa mali zake.

U T U M E K A T I K A M I J I

5. Maana yake: Utele wote na virutubisho vinavyotegemeza maisha ya mwanadamu kila mahali vimetolewa na Mungu bila kujali watu au upendeleo, Mt. 5:44-45 .

E. Wanadamu ni walengwa wa neema na kibali cha bure cha Mungu, kisicho na masharti. Yn. 3:16-17 – Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker