Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
458 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
1. Mungu alimpenda kila mtu katika dunia nzima, aliye hai, aliyekufa, na ambaye bado hata hajazaliwa pasipo vigezo wala upendeleo.
a. 2 Kor. 5:19
b. 1 Yoh. 4:9-10
c. Lk. 12:7
2. Thamani ya upendo wa Mungu inaonyeshwa katika dhabihu ya Mwanawe wa pekee kwa ajili ya kila mmoja, Mt. 18:14.
3. Mungu hakumtuma Mwanawe ili ahukumu, bali kuwaokoa wote waliomo duniani.
4. Maana: Neema ya Mwenyezi Mungu isiyo na mwisho na isiyo na kikomo iko juu ya kila mwanadamu, ingawa pengine hawajui .
4
U T U M E K A T I K A M I J I
F. Mungu anajihusisha na mapambano, mahitaji, na mizigo ya wale walio wanyonge zaidi na wenye kuumizwa miongoni mwetu. Zab. 146:5-9 – Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake, 6 Aliyezifanya mbingu na nchi, Bahari na vitu vyote vilivyomo. Huishika kweli milele, 7 Huwafanyia hukumu walioonewa, Huwapa wenye njaa chakula; Bwana hufungua waliofungwa; 8 Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki; 9 Bwana huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huipotosha.
1. Mungu ana mzigo kwa ajili ya wanadamu wanaoonewa, wenye njaa na wanaonyanyaswa kila mahali.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker