Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | KUT ENDA HAK I NA KUPENDA REHEMA : HAK I NA I SHUKE / 459

2. Bwana anajihusisha kikamilifu katika haki ya wale wanaoumia, yaani, walio vipofu na wenye kuinama.

3. Bwana anajua hatima ya wale wote ambao ni wakimbizi, wajane, yatima, na wasio na uwezo.

4. Dini katika utendaji wake safi kabisa mbele za Mungu inahusisha kuyajali mahitaji ya wale walio hatarini zaidi na wasioweza kujitetea na kujilinda wenyewe miongoni mwetu, Yak 1:27.

5. Maana yake: Mungu wa Yakobo kimsingi ni Mungu anayejihusisha na wanaoumizwa, maskini, na wanaokandamizwa .

G. Wanadamu wanaweza kubadilishwa na kufanywa upya kiasi cha kuwa washiriki wa asili ya kiungu. 2 Pet. 1:2-4 – Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu. 3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.

4

U T U M E K A T I K A M I J I

1. Kwa njia ya Kristo, waamini wamepewa mambo yote yanayohusu uzima na utauwa, 2 Pet. 1:3.

2. Mungu amewaita waliookolewa kwa utukufu na wema wake.

3. Kupitia ahadi kuu na za thamani za Mungu, tunaweza kuwa washiriki wa asili ya Mungu mwenyewe.

4. Waumini wameepukana na ufisadi uliomo duniani, unaochochewa na tamaa.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker