Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
46 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
2. Wakristo wanaofanya kazi ya kupamba na umaskini wanaweza kufika mahala wakaamini kwamba imani yao haitoshi kueleza dhuluma wanazokabiliana nazo kila siku.
B. Wakristo wengi wanatatizika kuelewa thamani na jukumu la kanisa la mahali pamoja linapokuja suala la umaskini.
1. Miundo Miwili ya Utume wa Mungu wa Ukombozi , Dk. Ralph Winter (Agosti, 1973)
a. Alifafanua aina mbili za mashirika (utaratibu wa kimfumo na shirika lisilo la kidhehebu) ambayo Mungu hutumia katika kila jamii ya wanadamu kufanya kazi kuelekea ukombozi.
2
b. Mashirika ambayo yamethibitisha thamani yao na kustahimili mtihani wa wakati, kama vile makanisa na madhehebu, yanachukuliwa kuwa utaratibu wa kimfumo.
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
c. Shirika lisilo la kidhehebu ni shirika linalolenga zaidi dhima iliyofafanuliwa kwa ufupi – namna ya utendaji ambayo Mungu hutumia katika kipindi fulani cha kihistoria, kama vile wakala au shirika la umisheni wa Kikristo, shirika lisilo la faida, au parachurch (shirika la kiimani lisilofungamana na dhehebu moja). d. Hitimisho la Dk. Winter lilikuwa kwamba njia bora zaidi kuelekea ukombozi ilikuwa ni taratibu za kimfumo (yaani makanisa na madhehebu) na mashirika yasiyo ya kidhehebu kufanya kazi kwa maelewano. Anapendekeza kwamba shughuli ya ukombozi ya Mungu inahitaji aina zote mbili za mashirika.
2. Kazi ya utetezi (advocacy) inapaswa kutazamwa kama njia yako rasmi au isiyo rasmi ya kuishi utume wa kanisa lako la mahali pamoja.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker