Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

462 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

C. Imago Dei katika kila mwanadamu ndio msingi wa kutenda haki na kupenda rehema.

1. Kwa hiyo, kataa kuzikubali dhana zozote za ulimwengu zinazosisitiza kukwepa uhalisia wa ulimwengu na mambo yake au zile zinazosisitiza haja ya kuufanania ulimwengu, huku ukimwomba Mungu akupe neema ya kuhusiana upya na ulimwengu kama mtu aliye ndani yake, lakini sio wa ulimwengu .

2. Thibitisha upekee na thamani ya maisha ya binadamu , katika ngazi zote, kuanzia kwa wale ambao hawajazaliwa, watoto wachanga na watoto, na wazee.

3. Ruhusu mtazamo wa kibiblia wa Mungu kama muumbaji na mwanadamu kama aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu kutafsiri upya “anthropolojia yako ya kitheolojia” (yaani, fundisho la ubinadamu) ili kukupatanisha na mtazamo wa juu na wa ajabu wa Biblia kuhusu wanadamu.

4. Kataa migogoro yoyote kati ya haki za kijamii, kupenda rehema, na uinjilishaji.

4

a. Tambua chanzo na lengo lake la pamoja.

U T U M E K A T I K A M I J I

b. Elewa jinsi yanavyomthibitisha Mungu kama muumbaji na mtawala wa ulimwengu.

c. Kataa kutofautisha (kugawanya na kutenganisha, kutengeneza mgongano kati ya) uinjilisti na haki za kijamii; vyote viwili vinahitajika katika kutoa ufahamu kamili kuhusu Mungu na Injili yake.

5. Mtazame kila mtu katika lenzi ya kushiriki kwake sura ya Mungu isiyo na kifani, ya pekee, na isiyo na mbadala na tazama kila fursa ya kumtunza na kumhudumia.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker