Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | KUT ENDA HAK I NA KUPENDA REHEMA : HAK I NA I SHUKE / 463

a. Kumtazama mwanadamu ni kutazama kitu cha thamani isiyo na mwisho.

b. Kumtazama mwanadamu aliyepondeka ni kumwona Bwana Yesu mwenyewe, Mt. 25:34-40.

Hitimisho • Uelewa wa kibiblia kuhusu imago Dei katika wanadamu huweka msingi na kuonyesha ulazima wa kujitolea kwetu kuwapenda, kuwathamini, na kuwalinda wanadamu, popote tuwakutapo na katika hali yoyote ile. • Kila mtu anastahili kutunzwa kwa sababu anashiriki imago Dei isiyo na kifani, ya kipekee, na isiyo na mbadala. Maswali yafuatayo yalikusudiwa kukusaidia kupitia maudhui ya video. Katika somo hili tuliona jinsi msingi wa utekelezaji wetu wa haki na kuonyesha rehema miongoni mwa maskini mjini ni kujitoa kwetu kwa uthibitisho wa kibiblia wa imago Dei katika kila mvulana, msichana, mwanamke na mwanamume. Kila mwanadamu, bila kujali rangi, asili, au utamaduni, anastahili kutunzwa kwa sababu anashiriki imago Dei isiyo na kifani, ya kipekee, na isiyo na mbadala. Kila binadamu na makundi yote ya binadamu ni ya kipekee na ya thamani. Wote ni wabebaji wa imago Dei na wanapaswa kutazamwa kama wa thamani na wasio na mbadala. Tafakari dhana hizi kupitia maswali yaliyo hapa chini, na uunge mkono hoja zako mwenyewe kwa kutumia Maandiko. 1. Toa ufafanuzi wa “sura ya Mungu” ( imago Dei ) uliotolewa katika somo. Ni kwa namna gani uthibitisho huu wa sura ya Mungu katika wanadamu ni uthibitisho wa kipekee na maalum? 2. Je, Maandiko yanatupa ufafanuzi wa wazi wa sura ya Mungu kwa wanadamu kama ilivyotajwa katika Mwanzo 1? Ni zipi baadhi ya tabia zinazotajwa kuwa ni za Mungu ambazo zinapatikana pia kwa wanadamu? 3. Je, mafundisho ya Biblia yanaelezaje ukweli kwamba wanadamu wote waliumbwa katika imago Dei ? Je, kuna wanadamu ambao, kwa sababu fulani, hawashiriki sura hii? Je, hata wanadamu waasi zaidi na wasio na dini wanashiriki imago Dei , bila kujali hali zao binafsi au za jamii zao,? Toa ushahidi wa kibiblia kwa jibu lako.

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

4

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker