Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

464 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

4. Kwa kuzingatia imago Dei , ni zipi baadhi ya njia ambazo Neno la Mungu linaeleza umuhimu wa imago Dei katika wanadamu? Ni kwa jinsi gani umuhimu huu unapaswa kubadilisha uelewa wetu kuhusu wanadamu, hata wale tunaowaona kuwa wa kuchukiza? 5. Maandiko yanafafanuaje mtazamo na hisia za Mungu kwa maskini, waliokandamizwa, na waliovunjika moyo? Je, hili lina umuhimu gani katika kuwaelewa maskini kama walengwa maalum wa kibali na neema ya Mungu ya bure na isiyo na masharti? Elezea jibu lako kwa kutumia Maandiko. 6. Je, kuna umuhimu gani katika ukweli kwamba wanadamu, bila kujali asili yao, wanaweza kubadilishwa na kufanywa upya kiasi cha kuwa washiriki wa asili ya uungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo? Je, wanadamu wote wanaweza kuja kushiriki asili hii mpya? 7. Nini kinaweza kusemwa juu ya wale wanaokataa zawadi ya neema ya Mungu katika Kristo – je, bado wanashiriki sura ya Mungu kama wanadamu wengine? Eleza. 8. Kwa kuzingatia maarifa yaliyo hapo juu, ni nini ungeona kuwa ndio msingi wa kutenda haki na kupenda rehema miongoni mwa maskini mjini? Je, ni kwa namna gani msingi huo unatuhabalisha kwa habri ya kufaa kwa kila mtu katika jiji, bila kujali tabia ya maisha na historia zao? Somo hili linaangazia theolojia na maono ya Ufalme, katika msingi wa Mungu kama Muumba wetu anayejali kwa habari ya ulimwengu na wale wanaoishi ndani yake. Pia tulizingatia nguvu ya sura ya Mungu ndani ya kila mtu, na jinsi sura hiyo inavyotumika kama msingi wa kutenda haki na kupenda rehema miongoni mwa maskini mjini. Ingawa Wakristo kiasili wamechukua misimamo tofauti kuhusiana na uhusiano kati ya Kanisa na ulimwengu, lazima tuhusiane nao. Kanisa ndio mahali pa Ufalme wa Mungu na wakala wake ulimwenguni lakini lenyewe si la ulimwengu. Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu ndiye Mungu wa asili, uumbaji, na hukumu, na pia Mungu wa wokovu, agano, na kuhesabiwa haki. Aidha, tuliona katika somo hili jinsi msingi wa kutenda haki na na kupenda rehema miongoni mwa maskini mjini ni uthibitisho wa imago Dei katika kila mvulana, msichana, mwanamke na mwanamume. Kila mtu anastahili kutunzwa kwa sababu anashiriki imago Dei isiyo na kifani, ya kipekee, na isiyo na mbadala. Pitia dhana hizi na zinazohusiana nazo katika orodha yake hapa chini.

UHUSIANISHAJI

4

Muhtasari wa Dhana Muhimu Ukurasa wa 196  6

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker