Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | KUT ENDA HAK I NA KUPENDA REHEMA : HAK I NA I SHUKE / 465
• Ufafanuzi mzuri wa imago Dei (yaani, sura ya Mungu) katika Maandiko, ni “Hali ya upekee wa wanadamu wote kwamba wameumbwa kama Mungu na kwa hivyo wanastahili heshima, ulinzi, na utunzaji wetu.” • Uthibitisho wa mwanadamu kuumbwa kwa mfano wa Mungu ni uthibitisho wa kipekee, hakuna kiumbe mwingine au malaika anayesemekana kuumbwa kwa mfano wa Mungu. • Ingawa namna maalum ambayo wanadamu wameumbwa kwa mfano wa Mungu haijasemwa waziwazi katika Maandiko, kuna uthibitisho unaoonyesha kwamba wanadamu wanashiriki sifa zinazolingana na za nafsi ya Mungu mwenyewe, yaani, haiba yetu, ufahamu wetu, uwezo wetu wa kuchagua, na uwezo wetu wa kimaadili. • Ukweli kwamba wanadamu waliumbwa katika imago Dei unadokeza kwamba wanadamu wote wanashiriki sura hii; kwa hiyo, wanadamu wote, bila kujali hali zao binafsi au za kijamii, ni wa pekee, wa thamani, na wenye thamani ndani yao. • Umuhimu wa kibiblia wa imago Dei katika wanadamu unabadilisha ufahamu wetu kuhusuu wanadamu. Wameumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyewe, wamevikwa taji ya utukufu na heshima, wameumbwa kwa namna ya kutisha na ya ajabu, na hustawishwa kwa upaji wa Mungu. Kwa namna hiyo, wanadamu wamefanywa kuwa walengwa wa kibali na neema ya bure ya Mungu , isiyo na masharti, na yeye mwenyewe anahusika na mapambano, mahitaji, na mizigo hata ya wanadamu walio wanyonge zaidi duniani. • Wanadamu, bila kujali historia zao, wanaweza kubadilishwa na kufanywa upya kiasi cha kuwa washiriki wa asili ya kiungu kupitia imani katika Yesu Kristo. Ingawa wale wanaomkataa Kristo hawashiriki katika kufanywa upya kwa sura hii ya Mungu, bado wanashiriki sura ya Mungu kama wanadamu wengine. • Msingi wa kutenda haki na kupenda rehema miongoni mwa maskini mjini ni uthibitisho wa imago Dei katika kila mvulana, msichana, mwanamke, na mwanamume. Kila mtu anastahili kutunzwa kwa sababu anashiriki imago Dei isiyo na kifani, ya kipekee, na isiyo na mbadala. Sasa ni wakati wa wewe kujadiliana na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu theolojia ya kutenda haki na kupenda rehema, na na kufikia kwenye kiini cha maana ya imago Dei kwa ajili ya kufanya huduma mjini. Ni wazi kwamba ni lazima tuweke msingi ufaao wa kitheolojia kabla ya kuchunguza viwango na vipengele
4
U T U M E K A T I K A M I J I
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi Ukurasa wa 197 7
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker