Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

466 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

mbalimbali vya huduma za huruma katika Kanisa. Kama mfuasi wa Yesu na kiongozi anayeibuka wa Kikristo, unahitaji kufahamu mawazo haya, na kuchunguza umuhimu wake kwa ajili ya maisha na huduma yako. Hii ndiyo fursa yako ya kuzingatia pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako binafsi kuhusu theolojia ya haki na mawazo ya imago Dei yaliyofafanuliwa katika somo hili. Maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuchunguza maswali yako mwenyewe, mahususi zaidi kuhusu maarifa haya. • Je, inawezekana kuamini kwamba Mungu ndiye Muumba wa mbingu na dunia na wakati huo huo kutoamini kwamba Mungu anajali ulimwengu na kila kinachoishi ndani yake? Eleza jibu lako. • Je, dhana ya ulimwengu kama kosmos ni dhana hasi au chanya katika Maandiko, au vyote viwili? (rej. Yn. 3:16 na 1 Yoh. 2:15-17). Tunajuaje kwamba Mungu anawapenda wakazi wa ulimwengu lakini anaupinga mfumo wa ulimwengu? • Kati ya maoni yote yaliyotolewa katika somo kuhusu uhusiano wa Kanisa na ulimwengu, ni yapi yanaleta maana zaidi kwako katika kujifunza kwako? • Je, kuna tatizo kubwa la kitheolojia kama tunalitazama Kanisa kama wakala wa Ufalme na sio Roho Mtakatifu kama wakala wa Ufalme? Je! nafasi ya Roho Mtakatifu katika Kanisa ni ipi watu wa Mungu wanapokuwa wakiuwakilisha Ufalme ulimwenguni? • Je, inadhoofisha kile tunachoamini ikiwa tunajaribu kusahihisha theolojia yetu kwa kusema kwamba Mungu ni Mungu wa asili yote na vile vile ni Mungu wa wokovu, Mungu wa uumbaji na vile vile Mungu wa agano, na Mungu wa haki na pia Mungu wa kuhesabiwa haki? Eleza. • Tulifafanua imago Dei (yaani, sura ya Mungu) katika Maandiko kama “Hali ya upekee wa wanadamu wote kwamba wameumbwa kama Mungu na kwa hivyo wanastahili heshima, ulinzi, na utunzaji wetu.” Je! Hii inamanisha kwamba hata watu waovu zaidi, wakatili, na wenye kuumiza zaidi wameumbwa kwa sura ya Mungu? • Je, kusema kwamba Mungu anawajali sana maskini na walioonewa haipingani na yale tunayojua kumhusu? Ikiwa ndivyo, tutaelewaje vifungu kama Mathayo 25 na “mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo” Bwana wetu aliowazungumzia? • Ikiwa wanadamu wote wameumbwa katika imago Dei , tunawezaje kuthubutu kuua binadamu yeyote, iwe kwa

4

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker