Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | KUT ENDA HAK I NA KUPENDA REHEMA : HAK I NA I SHUKE / 467
adhabu ya kifo au sheria ya jinai au vita? Je, imago Dei inamaanisha kwamba hakuna uhai wa mwanadamu unaopaswa kuondolewa kwa hali yoyote? Elezea jibu lako. • Kwa nini unafikiri kwamba Wakristo wengi hutetea misimamo kuhusu watu, ambayo inaonekana kwenda kinyume na umuhimu wa kibiblia wa imago Dei katika wanadamu? Ni katika hali gani (kama zipo) tunaweza kuhalalisha kuwatendea wanadamu wengine kama maadui zetu? Eleza. • Itakuwaje kama nimekua nikiwa sina upendo na jamii au kundi fulani. Je, inawezekana kuvumilia chuki au ubaguzi wowote na bado kudai kuwa washiriki wa asili ya kiungu kupitia imani katika Yesu Kristo? • Je, ni kwa namna gani kuthibitisha imago Dei katika kila mvulana, msichana, mwanamke, na mwanamume katika kundi usilothamini kunaweza kubadilisha mawazo na hisia zako kwa kundi hilo au watu hao? Vipi kama kuthibitisha ukweli huo kuhusu wao hakutapelekea katika hisia zilizobadilika kuwahusu – nini kitafuata? Kwenda Mbali Kidogo na Mambo Haya Mjadala mkubwa sasa unaendelea kanisani juu ya uamuzi wa hivi karibuni wa mzee fulani kuanzisha Nyumba Maalum ya Wanaume kwa ajili ya watu waliowahi kuwa wafungwa, na kuwasaidia kuhitimu kurudi katika jamii. Mmoja wa washirika wa kanisa aliyekuwa na maono, mzigo, na ujuzi wa kuanzisha huduma hiyo, aliwashirikisha wazee mzigo wake, na kwa zaidi ya miezi tisa walichunguza mzigo wake na kugundua kuwa ni wa dhati na unaendana na mkakati wa kanisa. Hata hivyo, kundi fulani la kanisa linalozidi kuongezeka, limekuwa na mashaka juu ya uhalali wa wazo hilo tangu mwanzo. Je, wangewezaje kuhakikisha usalama wa washirika wengi wa kanisa huku wanaume hawa wakionekana mara nyingi katika ibada na shughuli za kanisa? Baadhi ya wanaume hawa walikuwa na historia ya uhalifu wa kingono, na familia nyingi zenye vijana zimeelezea kusikitishwa kwao na wasiwasi wao juu ya uwepo wa watu kama hao katika ushirika wa kanisa. Wengine walitetea kwa msisitizo kwamba neema ya Mungu inaweza kuwabadilisha, na kwamba wanadamu wote, bila kujali historia, wanaweza kubadilishwa kwa neema ya Mungu katika Kristo. Matarajio ya kuanzisha huduma hiyo yamezua uvumi kuhusu kuondoka kwa watu wengi kanisani kama wazo hilo likiendelea. Kama ungekuwa mchungaji kiongozi katika kusanyiko kama hilo, ungeichukuliaje huduma hii, hasa katika mwangaza wa maarifa yaliyotolewa katika somo hili kuhusu kanisa, imago Dei , na kanisa kama eneo na wakala wa Ufalme wa Mungu? Eleza jibu lako.
MIFANOHALISI
1
4
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker