Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
468 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Hakuna Vita Tena Kwa kuzingatia machafuko mengi, mapambano, mapigano ya silaha, na migogoro mbalimbali inayoendelea katika sehemu nyingi za ulimwengu leo, sisi kama Wakristo lazima tuelewe msimamo wetu kuhusu vita na vurugu. Ikiwa Mungu ni Mungu wa kuhesabia haki kwa imani na pia Mungu wa haki, basi inawezekana kuzungumzia vita na migogoro ambayo ni ya haki. Katika historia yote ya Kanisa, Wakristo wacha Mungu, wanyofu, na wa kibiblia wamekuwa wakipingana kuhusu uhalali wa vita kuwa suluhu ya migogoro, uhalali wa Wakristo kutumika vitani, hata uhalali wa Wakristo kuwa katika jeshi. Kama kawaida mistari huchorwa kwa uwazi sana. Upande mmoja unaweka msisitizo kwamba Wakristo wamekatazwa kuwaua wengine, kwa kuwa wanadamu, wote ni wa thamani machoni pa Mungu, na wameumbwa kwa sura yake. Wengine hudai kwamba mamlaka zilizopo zipo kwa mamlaka ya Mungu, na maandiko mengi yanahimiza Mkristo amheshimu mfalme, anyenyekee kwa mamlaka zinazotawala, na kutumikia taasisi zinazoongoza kwa staha na heshima. Je, sisi kama waamini tuko mbali kiasi gani katika kulibeba fundisho hili kuhusu imago Dei , hasa linapokuja suala la kuhudumu katika tawi fulani la huduma za kijeshi nchini? Je, tunaweza kuthibitisha imago Dei na bado tukatumika katika jeshi, katika nafasi ambayo itatuhitaji kutoa uhai wa binadamu? Imago Dei na Adhabu Kifo Mojawapo ya utata endelevu miongoni mwa jumuiya nyingi za Kikristo ni suala la adhabu ya kifo. Waamini wengi leo hii wanashikilia msimamo kwamba kwa kuwa wanadamu wote wameumbwa katika imago Dei , haturuhusiwi kumuua mwanadamu yeyote, hata kama mtu huyo amethibitishwa kuwa na hatia ya kosa jinai linalopelekea adhabu ya kifo. Wengine, wakinukuu maandiko yale yale, wanaamini kwamba ili serikali izuie uovu na kuimarisha haki, adhabu ya kifo ni muhimu na inasaidia. Wanadai kwamba sio tu kwamba inatekeleza haki kwa mhusika wa uhalifu, lakini pia inatumika kama ukumbusho kwa wengine juu ya matokeo ya tabia kama hiyo ya uhalifu. Unasemaje kuhusu uhalali wa adhabu ya kifo, na uthibitisho kwamba wanadamu wote (hata wenye hatia) wameumbwa kwa imago Dei ? Je, hili linapaswa kuleta mabadiliko katika kile tunachofikiri kuhusu adhabu ya kifo?
2
3
4
U T U M E K A T I K A M I J I
Nipe Muda, Bado Nakua Wakati ni wachache wangepinga agizo la wazi la kibiblia la kuwapenda wengine kama Kristo alivyotupenda sisi kama ishara inayotambulisha ufuasi wa kweli (Yn. 13:34-35), wengi hubishana
4
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker