Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | KUT ENDA HAK I NA KUPENDA REHEMA : HAK I NA I SHUKE / 469

kuhusu namna ambazo upendo huo unapaswa kudhihirishwa, na vilevile ni wakati unaofaa kuudhihirisha. Mkristo mpya ambaye katika maisha yake yote alikuwa amefundishwa kuchukia watu wa jamii fulani hakushawishika kabisa kubadili hisia na mawazo yake kuelekea kwenye msimamo wao. Uongofu wake na imani yake katika Yesu Kristo ilionekana kwa kila namna kuwa ya dhati na halisi, lakini mashaka yake endelevu, chuki, na kutoamini wengine wa jamii nyingine vilidumu kwa miezi kadhaa, na mwongofu huyo mpya hakuficha dharau yake na chuki yake ya wazi kwa “watu hao.” Ingawa wengine waliamini kwamba tabia yake endelevu ilikuwa ishara ya kushindwa kuokoka kiukweli, wengine waliona ni masalio ya maisha yake ya zamani na waliitazama tu kama eneo la yeye kukua. Walisisitiza kwamba, watoto wote wachanga waliozaliwa katika Kristo, watakuwa na maeneo katika maisha yao ambayo yanahitaji wakati wa kuvua utu wa kale, kufanywa upya katika roho ya nia zao, na kuvaa utu mpya ulioumbwa kwa namna ya Mungu kwa mfano wa utakatifu wa kweli na haki. (rej. Efe. 4:20-). Je, unafikiri nini kuhusu hali hii – je, kushindwa kupenda katika hali ya namna hii ni jambo la kawaida katika ukuaji wa Kikristo, au ni ishara ya kushindwa kutubu? Je, viongozi katika hali kama hii wanawezaje kujua lipi hasa ni tatizo? Kama aliyeifanya na kuiumba dunia, Mungu wetu anahusika kikamilifu na ulimwengu na wale wanaoishi ndani yake. Kiasili, jumuiya za Kikristo zimekuwa na mitazamo mbalimbali kuhusu ulimwengu, ikiwa ni pamoja na kujiondoa katika ulimwengu, kuishi katika mvutano na ulimwengu, au kukubali jukumu la kuubadilisha. Kanisa ni eneo na wakala wa Ufalme wa Mungu ulimwenguni lakini sio la ulimwengu. Kwa hivyo, Kanisa linathibitisha kwamba Mungu ni Mungu wa asili yote na vile vile Mungu wa wokovu, Mungu wa uumbaji na vile vile Mungu wa agano, na Mungu wa haki na vile vile Mungu wa kuhesabia haki. Katika huduma yake kama mwakilishi wa Ufalme wa Mungu, Kanisa limeitwa kudhihirisha na kutangaza uhuru kwa ulimwengu, limeitwa kudhihirisha ukamilifu wa Mungu ulimwenguni na kusimama kwa ajili ya haki ya Mungu ulimwenguni kote. Msingi wa kutenda haki na kupenda rehema miongoni mwa maskini mjini ni uthibitisho wa imago Dei katika kila mvulana, msichana, mwanamke, na mwanamume. Kila mtu anastahili kutunzwa kwa sababu anashiriki imago Dei isiyo na kifani, ya kipekee, na isiyo na mbadala. Kwa sababu wameumbwa kwa mfano wa Mungu, wanadamu wote ni wa pekee na wenye thamani. Sura hiyo ni msingi wa sababu ya kwa nini tunapaswa kutenda haki na kupenda rehema miongoni mwa watu binafsi, familia, makabila, na mataifa yote duniani. Kila moja wao kama abebaye imago Dei anapaswa kuchukuliwa kuwa ni wa thamani na asiye na mbadala.

Marudio ya Tasnifu ya Somo

4

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker