Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
470 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Ikiwa ungependelea kufuatilia baadhi ya mawazo ya Haki na Ishuke: Maono na Theolojia ya Ufalme , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Cone, James. The God of The Oppressed . New York: Seabury Press, 1975. Conn, Harvie. Evangelism: Doing Justice and Preaching Grace . Grand Rapids: Zondervan, 1982. Fletcher, William M. The Second Greatest Commandment: A Call to A Personal and Corporate Life of Caring . Colorado Springs: NavPress, 1983. Kirk, Andrew. The Good News of the Kingdom Coming: The Marriage of Evangelism and Social Responsibility . Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1983. Sehemu hii ni fursa mahususi kwako kutafuta uongozi wa Roho Mtakatifu kuhusu matumizi yako mahususi ya maarifa ya somo hili. Uwezo huu wa kusikiliza na kufuata msukumo wa Roho Mtakatifu ni muhimu katika mchakati wowte wa kujifunza, mazungumzo, na unyenyekevu. Sasa hii hapa ni nafasi yako ya kugundua kwa njia ya kutafakari na maombi uhusiano wa theolojia hii ya juu na huduma yako halisi kadhalika na maisha yako kwa ujumla. Uwanda wa matumizi haya unaweza kuwa leo, wiki hii, mwezi huu, au hata mwaka mzima. Yote haya yanategemea kile unachohitaji kujua na kile ambacho Roho Mtakatifu anataka utumie katika maisha na huduma yako. Kwa hiyo, chukua muda kusubiri mbele za Bwana na kumsikiliza Roho Mtakatifu katika maombi ya wazi. Je, anaonekana kudokeza nini kwako kuhusu ufahamu wako mwenyewe juu ya umuhimu wa haki na rehema katika maisha yako, katika mahubiri yako na mafundisho, katika huduma yako kanisani, na majirani zako? Je, Bwana anakuletea akilini mwako mtu fulani, hali, au tukio akikutaka wewe ufanye jambo katika mwangaza wa mafundisho ya somo hili? Je, Roho Mtakatifu anaonekana kukusukuma kubadili kitu katika maisha na huduma yako, au pengine kuanza au kuanzisha jambo fulani? Ahadi kutoka katika Neno la Mungu ni hakika: baraka huja kwa mtu ambaye hasikii tu Neno, bali analitenda (Yak. 1:22 25). Kuwa wazi kwa Roho unapochunguza maana mbalimbali za mafundisho haya kwa ajili ya maisha na huduma yako.
Nyenzo na Bibliografia
Kuhusianisha Somo na Huduma
4
U T U M E K A T I K A M I J I
Nguvu ya maombi ni muhimu kwa ajili ya maendeleo yetu kama wanafunzi wa Kristo na viongozi wa Kanisa. Kujifunza kushiriki maombi na wanafunzi na viongozi wenzako kutaimarisha kila awamu ya ukuaji wako katika Kristo. Bila shaka, hakuna mtu anayeweza kusoma mawazo yako; utahitaji kuwa wazi kuhusu
Ushauri na Maombi
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker