Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | KUT ENDA HAK I NA KUPENDA REHEMA : HAK I NA I SHUKE / 471
njia ambazo unatafuta neema ya Bwana ili kuzitumia kweli hizi na kuzihusianisha na mwenendo na huduma yako mwenyewe. Zaidi ya hayo, wakufunzi wako wapo tayari zaidi kukupa ushauri, na maarifa kuhusu masuala na hali fulani ambazo huenda unakabiliana nazo. Kuwa wazi kupokea ushauri wa viongozi wako kadiri unavyoshughulikia changamoto mbalimbali zinazokukabili siku ya leo, na hakikisha unawaomba wanafunzi wenzako wakuinue katika maombi huku ukitafuta kufanya kweli ulizochimba katika somo hili kuwa hazina yako ya kudumu. Kumbuka maneno ya Bwana wetu anapofundisha juu ya nguvu ya maombi: Mt. 7:7-11 – Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; 8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. 9 Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? 10 Au akiomba samaki, atampa nyoka? 11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao? Ukiwa na hisia hii ya kutiwa moyo akilini, mwombe Bwana akupe ufahamu wa kina katika maana ya kweli hizi, pamoja na fursa na nguvu za kuliitikia Neno la Mungu kwa upesi na kwa utii katika maisha yako. Washirikishe wanafunzi wenzako mahitaji yako na mwombeane. Kuomba kwa mwenye haki ni jambo lenye nguvu, hakika (Yak. 5:16)!
KAZI
4
Amosi 5:20-24
Kukariri Maandiko
U T U M E K A T I K A M I J I
Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/ books ili kujua kazi ya kusoma ya juma lijalo, au muulize Mshauri wako.
Kazi ya Usomaji
Wakati huu ni muhimu uwe umeainisha na kuthibitisha mapendekezo yako kuhusu kazi yako ya huduma kwa vitendo, na iwe imepitishwa na mkufunzi wako. Hakikisha kwamba unapanga shughuli zako mapema, ili usichelewe kukabidhi kazi zako.
Kazi Zingine Ukurasa wa 198 8
Hongera kwa kukamilisha Mtaala wa Cornerstone! Ni maombi yetu kwamba mafunzo uliyopata kupitia masomo haya kumi na sita yakuwezeshe kumtukuza Mungu kwa kumtumikia Kristo na Kanisa
Unapokamilisha Somo Hili la Mwisho
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker