Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
48 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
• Viashiria vya kazi hatarishi ya kupambana na umaskini ni “ugonjwa wa mwokozi”, hali ya ubaba, uchovu sugu, na ubeuzi. • Kuna thamani ndogo katika kujadili kuhusu sababu za kwa nini watu ni maskini. • Sababu kuu ya watu nchini Marekani kuwa katika umaskini ni mazingira ya ajira ambazo hazilipi vya kutosha. • Mungu ni mkuu kuliko hali ya umaskini.
Sasa ni wakati wako wa kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu somo letu, Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini . Je, una maswali gani, ukizingatia mambo ambayo umejifunza hivi punde?
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
MFANOHALISI
Baada ya kukamilisha somo hili, rejea mfano halisi ulioelezwa hapo awali katika somo hili. Je, unaweza kutoa jibu gani la tofauti, kwa kuzingatia maudhui ya somo hili? Baadhi ya marafiki wanakuomba utembelee ghala la Kikristo la kugawa chakula kwa wahitaji, ambapo wanafanya kazi kwa kujitolea. Kama mtu wanayemwamini, wanataka uangalie na utoe maoni yako juu ya utendaji wa ghala hiyo. Jambo la kwanza unaloona unapotembea ni baadhi ya watu walio vifua wazi wakicheza kamari, kuvuta sigara na kunywa pombe karibu na mlango. Unapoingia ndani, unashangazwa na jinsi ndani palivyo giza na pachafu. Mambo yanaonekana yamekaa shaghalabaghala na huwezi kujua ni kwa namna gani watu wanavyopokea mahitaji yao. Watu wanachoka kusubiri. Kisha mhubiri kijana anakuja katika eneo la kungojea na kutoa mahubiri. Anapomaliza, kila mtu anainua mkono wake kumpokea Kristo. Baada ya kama saa moja hivi, mtu wa kwanza anaenda mbele kuchukua mfuko wa vyakula, jambo hilo linageuka kuwa mzozo mkubwa kati ya mtoa huduma na mteja juu ya uchaguzi wa chakula. Mtoa huduma anamwambia kwamba alichokipata ndicho kilichotolewa, na anapaswa kufurahiya. Baadaye, unatoka kwenda kula chakula cha mchana na marafiki zako ili kujadili uchunguzi wako. Unaweza kuwaambia nini?
2
Ukurasa wa 35 8
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker