Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | KAZ I HATAR I SH I YA KUPAMBANA NA UMASK I N I / 49
Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini inaelezea aina ya kazi ya kupambana na umaskini ambayo kwa asili hutokana na asili yetu ya dhambi. Ili kujitambua zaidi kwa habari ya mielekeo yetu ya upendeleo na ubaguzi, ni lazima tufanye upya fikra zetu kuhusu kazi tuifanyayo katika kupambana na umaskini, tukubali ni wapi tumeshiriki katika kufanya kazi ya kupambana na umaskini kwa namna hatarishi, na kutambua viashiria vya kazi hatarishi ya kupambana na umaskini. Ikiwa una nia ya kufuatilia kwa kina baadhi ya mawazo kutoka kwa somo hili, Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Sanders, Alvin. Bridging the Diversity Gap . Indianapolis: Wesleyan Publishing House, 2013. Davis, Don L. Winning the World: Facilitating Urban Church Planting Movements , Foundations Course, Wichita: TUMI, 2007, 2012. Davis, Don L. Get Your Pretense On! Wichita: TUMI, 2018. Chukua muda kutafakari jinsi Roho Mtakatifu anavyoweka muunganiko kati ya maarifa ya somo hili la Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini na maisha na huduma yako. Je, unawezaje kufikiria, au kutenda tofauti katika hali halisi kulingana na somo hili? Je, somo hili linakufanya ufikirie upya mawazo au matendo yako ya awali? Omba kwamba Bwana wetu akuonyeshe mifano au mazingira halisi ya maisha yako mwenyewe ambapo somo hili linaweza kutumika.
Marudio ya Tasnifu ya Somo
Nyenzo na Bibliografia
2
Kuhusianisha Somo na Huduma
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
Mwambie Roho Mtakatifu auangazie moyo wako kuhusu Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini . Jitoe upya kwa utumishi kwa Bwana wetu kama mfanyakazi wa kiukombozi dhidi ya umaskini. Mwombe akupe ufahamu na ujasiri wa kutumia yale unayojifunza.
Ushauri na Maombi
KAZI
Kariri Yohana 1:14 kwa kutumia Biblia, tafsiri ya kawaida (SUV).
Kukariri Maandiko
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker