Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | KAZ I YA K I UKOMBOZ I DH I D I YA UMASK I N I / 51

Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini

S OMO L A 3

Ukurasa wa 37  1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maarifa ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kufanya upya uelewa wako wa dhana ya ukombozi. • Kutafakari jinsi kazi yako ya kupambana na umaskini inaweza kuwa ya ukombozi. • Kutofautisha kazi ya kiukombozi dhidi ya umaskini na aina nyinginezo. Omba sala ifuatayo: Bwana, tufundishe kuisikia sauti yako. Wakati wa huzuni unapofika, tusaidie tuhuzunike. Wakati wa kushangilia unapofika, tusaidie tushangilie. Tunapochoka, uwe nguvu katika udhaifu wetu. Na mapenzi yako mazuri na makamilifu, sio yetu, yafanyike. Amina. Soma Yohana 1:1-8 . Tafakari na andika kanuni zinazoweza kutendewa kazi katika maisha. Hitimisha sehemu hii kwa kusikiliza “Wewe ni Mungu” na utafakari Maandiko ambayo umesoma hivi punde. Kama mtu ambaye nimeishi katika jamii ya watu maskini wanaofanya kazi, na pia kuhudumu miongoni mwao, ninaelewa jinsi ukombozi ulivyo muhimu. Ninajua jinsi unavyotamani kuwa na maisha bora. Nimehisi uzito wa kuwa sehemu ya jamii iliyoharibikiwa. Mwanzo 3 (Anguko) kweli lilitokea, na wale wanaoishi katika hali ya umaskini wanaishi matokeo yake kila siku ya maisha yao. Ni mada ya kawaida katika sinema kwamba shujaa yuko tayari kufa kwa ajili ya kusudi fulani. Hata hivyo, ukweli ni kwamba ni watu wachache sana wako tayari kwenda mbali kiasi hicho. Tunamjua mtu ambaye alikuwa na utayari huo – Yesu Kristo. Kwa bahati mbaya, wengi wetu tumepunguza upana, kina na uzito wa hadithi yake katika maelezo mafupi ya “Mungu aliumba ulimwengu, sisi ni wenye dhambi, na kwa sababu hiyo Mungu alimtuma Yesu ili atuokoe kutoka katika dhambi zetu.” Uumbaji ~ Common Prayer: A Liturgy for Ordinary Radicals.

Malengo ya Somo

Ibada

3

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker