Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
52 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
dhambi-Yesu, basi. Je! ni nini kibaya katika ufupisho huu? Hakuna, isipokuwa, hayajakamilika. Vitabu vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana vinajulikana kama Injili. Viliandikwa ili kutumika kama zana za uinjilisti. Kimsingi, neno “Injili” linamaanisha habari njema. Ni kwa kusoma vitabu hivi ambapo tunapata wazo hili kwamba Yesu Kristo alifanyika fidia kwa ajili ya dhambi zetu. Sote tulikuwa wafungwa wa dhambi, alilipa gharama ya fidia kwa ajili ya uhuru wetu, na hili lilitupatia sisi wanadamu maisha mapya. Neno tunalotumia kuelezea mchakato huu ni ukombozi. Ukombozi unahusisha dhabihu kwa kusudi la urejesho. Hadithi nzima ya kifo, kuzikwa, na kufufuka kwa Yesu Kristo ni ya kina zaidi kuliko ufupisho ambao mara nyingi tunaufanya kuelezea hadithi hiyo. Kazi ya ukombozi ya Kristo ilianzisha wazo la kubadilisha ulimwengu kwamba Shetani ameshindwa, kazi za ibilisi zinaharibiwa, na utawala wa Mungu umewekwa tena hapa duniani. Hadithi nzima inatangaza kwamba Mfalme yuko hapa! Kuna njia tofauti za kuitazama dhambi. Linapokuja suala la umaskini, mtazamo mkuu unapaswa kuwa kwamba dhambi ni kandamizi. Kwa sababu ya dhambi, watu wengi sana wana maisha duni. Tunawafanya watu walio katika umaskini kuwa duni ikiwa hatutawajulisha ukweli kwamba kazi ya ukombozi ya Kristo inaashiria ushindi dhidi ya nguvu za dhambi na uovu.
3
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
Tamka na/au imba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho).
Kanuni ya Imani ya Nikea
Kariri Yohana 1:14 kwa kutumia Biblia ya kawaida (si toleo lililofafanuliwa), kisha ujisahihishe mwenyewe kwa kutumia Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko.
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, rejelea ratiba ya kozi hii ili kuona kazi zinazopaswa kufanyika kabla ya mkutano wako ujao wa darasa na ukamilishe kazi zilizo hapa chini: Soma yafuatayo: • Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini – “Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini” (uk. 31-36)
Kazi
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker