Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | KAZ I YA K I UKOMBOZ I DH I D I YA UMASK I N I / 53

• Kanisa Lisilo la Kawaida: Mabadiliko ya Jamii kwa Manufaa ya Wote – Sura ya 4: Watu wa Mungu: Mpango wa Mungu kwa Ulimwengu Ulioharibika – Sura ya 8: Kupambania Jamii: Uwawezeshaji wa Viongozi na Wafanyakazi Mashinani – Sura ya 10: Ufalme Uko Ndani Yetu Andika muhtasari wa kila usomaji wa kitabu kwa maneno yasiyozidi aya moja au mbili kwa kila muhtasari. Katika muhtasari huu, tafadhali toa uelewa wako bora zaidi wa kile unachofikiri kilikuwa jambo kuu katika usomaji. Usijali sana juu ya kutoa maelezo; andika tu kile ambacho unaona kuwa jambo kuu linalozungumziwa katika sura hiyo ya kitabu. Tumia Fomu ya Ripoti ya Usomaji. Wasilisha Fomu uliyojaza kwa ajili ya kila kitabu (ikiwa unasoma kozi hii kwa kutumia World Impact U, tumia upau wa kijani wa “Wasilisha Kazi” juu ya ukurasa wowote katika kozi yako ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini katika WIU). Mfano Halisi Umekuwa ukifanya kazi na Sheri kwa miaka mitano. Kwa maelezo yote, Sheri ni mwanamke mzuri na mwenye imani thabiti. Yeye huhudhuria kanisani kila Jumapili ambayo hajapangiwa kufanya kazi katika hoteli kama mhudumu. Mara zote huleta nyumbani pesa za kutosha kujikimu yeye na watoto wake watatu, kwa kuwa baba yao hachangii sana. Hivi sasa, amekasirika kwa sababu amegundua kwamba mmoja wa wanawe amefukuzwa kutoka kwenye shule binafsi ya Kikristo ambayo wewe ulichangia sana kuandikishwa kwake hapo. Kwa upande mmoja, anahisi kuaibishwa; kwa upande mwingine, anahisi ni kama haonekani mbele za Mungu kwa sababu, kwa maoni yake, shule imeyafanya hayo kwa sababu za ubaguzi wa rangi na tabaka la kijamii analotokea. Unadhani utamweleza nini Sheri?

KUJENGA DARAJA

3

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini

Dr. Alvin Sanders

MAUDHUI

Somo la tatu, Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , inafafanua lengo la shughuli zetu. Tutachunguza aina tatu za kazi ya kupambana na

Muhtasari

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker