Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 3 | KAZ I YA K I UKOMBOZ I DH I D I YA UMASK I N I / 55
B. Mtazamo wa Kimaadili: hatua katika mwelekeo sahihi (Ezra 1:1-11, 6:1-12).
1. Mkazo ni juu ya uhusiano kati ya watenda kazi wa kupambana na umaskini na wanufaika (walengwa) kila inapowezekana.
2. Mtazamo wa kimaadili unaweza kufanya mengi mazuri kwa jamii yetu kwa kutafuta manufaa ya wote.
C. Mawazo ya Ukombozi: kuwapenda jirani zetu kama nafsi zetu (Ruthu 1:15-18, 3:9-13)
1. Mawazo ya ukombozi ni urejesho wa uumbaji kupitia dhabihu.
2. Mtazamo wa ukombozi unasema, “Ninajitolea, tunashinda.” Mtazamo huu unajumuisha wanufaika wa kazi yetu na jinsi tunavyotumia rasilimali.
3
3. Ni kuwapenda jirani zetu kama nafsi zetu. Ni jinsi tunavyounganisha hadithi yetu na hadithi ya Mungu.
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
II. Kazi ya Kiukombozi katika Biblia
Ukurasa wa 40 3
A. Kupitia kifo chake, Kristo alilipa gharama ya maisha yetu ili kutufungua kutoka katika kifungo cha dhambi. Halikuwa tu tukio lililopita bali ni tumaini lililopo daima, linaloendelea (Warumi 5:18-21).
B. Dhamira ya ukombozi inayopatikana katika Biblia kihistoria imeambatanishwa na dhana ya Christus Victor ; Kristo alikuja kufa kwa ajili ya dhambi, kumshinda Shetani na kuharibu kazi zake, na kuwakilisha utawala wa Mungu duniani (Kol. 2:13-15; Ebr. 2:14-15; 1 Yoh. 3:8).
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker