Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
58 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Umekuwa ukifanya kazi na Sheri kwa miaka mitano. Kwa maelezo yote, Sheri ni mwanamke mzuri na mwenye imani thabiti. Yeye huhudhuria kanisani kila Jumapili ambayo hajapangiwa kufanya kazi katika hoteli kama mhudumu. Mara zote huleta nyumbani pesa za kutosha kujikimu yeye na watoto wake watatu, kwa kuwa baba yao hachangii sana. Hivi sasa, amekasirika kwa sababu amegundua kwamba mmoja wa wanawe amefukuzwa kutoka kwenye shule binafsi ya Kikristo ambayo wewe ulichangia sana kuandikishwa kwake hapo. Kwa upande mmoja, anahisi kuaibishwa; kwa upande mwingine, anahisi ni kama haonekani mbele za Mungu kwa sababu, kwa maoni yake, shule imeyafanya hayo kwa sababu za ubaguzi wa rangi na tabaka la kijamii analotokea. Unadhani utamweleza nini Sheri? Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ndio lengo na kusudi la kazi yetu ya kupambana na umaskini. Kazi hii inatofautiana sana na mifumo na utendaji wa Kiunyonyaji na wa Kimaadili. Kupitia ufahamu wetu wa kazi ya Kristo msalabani, sasa tunaweza kuitikia kwa njia inayoakisi ukombozi katika namna tunavyowatendea wengine, tukiwa na matarajio mapya kupitia mfumo wenye msingi wa ukombozi kuelekea watu wanaoishi katika mitaa yenye umaskini. Ikiwa una nia ya kufuatilia kwa kina baadhi ya mawazo kutoka kwa somo hili, Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Sanders, Alvin. Bridging the Diversity Gap . Indianapolis: Wesleyan Publishing House, 2013. Davis, Don L. Kutenda Haki na Kupenda Rehema: Huduma za Huruma na Upendo , Moduli ya 16 ya Capstone, Wichita: TUMI, 2005. Engel, Bob. Mere Missions: Moving Forward to Multiply , Wichita: TUMI, 2022. Chukua muda kutafakari jinsi Roho Mtakatifu anavyoweka muunganiko kati ya maarifa ya somo hili la Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini na maisha na huduma yako. Je, unawezaje kufikiria, au kutenda tofauti katika hali halisi kulingana na somo hili? Je, somo hili linakufanya ufikirie upya mawazo au matendo yako ya awali? Omba kwamba Bwana wetu akuonyeshe mifano au mazingira halisi ya maisha yako mwenyewe ambapo somo hili linaweza kutumika.
Marudio ya Tasnifu ya Somo
3
Nyenzo na Bibliografia
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
Kuhusianisha Somo na Huduma
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker