Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | MI ENENDO YA MA I SHA NA KAZ I YA KUPAMBANA NA UMASK I N I / 63

– Sura ya 5: Ushirika wa Kanisa wenye Afya: Tabia Saba kuelekea Ukomavu wa Kiroho – Sura ya 9: Kufuata Ndoto Zisizo za Kawaida: Mifano ya Imani, Matumaini, na Upendo kwa Vitendo. Andika muhtasari wa kila usomaji wa kitabu kwa maneno yasiyozidi aya moja au mbili kwa kila muhtasari. Katika muhtasari huu, tafadhali toa uelewa wako bora zaidi wa kile unachofikiri kilikuwa jambo kuu katika usomaji. Usijali sana juu ya kutoa maelezo; andika tu kile ambacho unaona kuwa jambo kuu linalozungumziwa katika sura hiyo ya kitabu. Tumia Fomu ya Ripoti ya Usomaji. Wasilisha Fomu uliyojaza kwa ajili ya kila kitabu (ikiwa unasoma kozi hii kwa kutumia World Impact U, tumia upau wa kijani wa “Wasilisha Kazi” juu ya ukurasa wowote katika kozi yako ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini katika WIU). Mfano Halisi Unafanya Kazi ya Kupambana na Umaskini katika mitaa ya jirani hapo mjini na unakutana na mwenzako kwenye duka lililopo kwenye kona. Anakuuliza kama una muda wa kutosha wa kuzungumza. Baada ya kutembea hadi ofisini kwake na kuanza kuzungumza, ni dhahiri kuwa ana hasira na ni mwenye kuchanganyikiwa. Amelemewa na changamoto anazokabiliana nazo kila siku. Changamoto hazikushtui kwa sababu hata wewe unakutana nazo. Hata hivyo, kinachokushtua ni sauti yake na kile anachosema. Anahisia za kibeuzi sana kwa habari ya watu wa mitaa hiyo na mashirika yaliyoanzishwa ili kuwasaidia, ikiwa ni pamoja na kanisa lake la mahali ambalo ameacha kuhudhuria. Malalamiko yake yanahusu kutothaminiwa kwa namna alivyojitoa na jinsi alivyochoka kimwili. Ungemwambia nini?

KUJENGA DARAJA

4

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini

Dk. Alvin Sanders

MAUDHUI

Somo hili la Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini , linaweka wazi hali ya kiroho ya Mapokeo Makuu ya Kanisa. World Impact inakualika kutendea kazi maarifa haya katika maisha yako kama njia ya kukabiliana na kazi hatarishi ya kupambana na umaskini, na kuyafanya kuwa kichocheo cha kukua katika imani yako.

Summary Ukurasa wa 46  2

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker