Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
64 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Malengo yetu ya somo hili, Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini , ni kukuwezesha: • Kufanya upya ufahamu wako kuhusu hali ya kiroho yenye ufanisi. • Kutafakari kuhusu utendaji kazi wa muunganiko kati ya mazoezi ya kiroho na kazi ya kupambana na umaskini. • Kuweka ahadi za msingi kwa habari mazoezi ya kiroho yaliyomo katika Mapokeo Makuu ya Kanisa. Yesu anasema maisha yetu ya Kikristo yanahusu – kumpenda Mungu na kuwapenda watu (Mt. 22:37-40). Fikiria amri hizi kama sehemu mbili za kwanza za dhima ya maisha yetu. Kama watenda kazi wa kupambana na umaskini, pia tuna sehemu ya tatu, ya kipekee. Tumechagua kupeleka vipaji vyetu, vipawa vya kiroho, na pesa ili kuboresha hali ya maisha ya wale wanaoishi katika umaskini na jamii ya zao.
I. Mapokeo Makuu na Kazi ya Kupambana na Umaskini
Muhtasari wa Maudhui ya Video
A. “Mapokeo Makuu yanawakilisha kiini kikuu cha misingi ya imani na desturi za Kikristo zinazotokana na Maandiko ambazo zilitawala kati ya wakati wa Kristo na katikati ya karne ya tano” (Dk. Don Davis, Sacred Roots , TUMI: 2010, p. 74) .
4
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
B. World Impact inashikilia nidhamu manane kama njia dhahiri za kukabiliana na sumu ya “ugonjwa wa mwokozi”, hali ubaba, uchovu sugu, na ubeuzi unaopatikana ndani ya kazi ya kupambana na umaskini.
II. Muhtasari wa Nidhamu za Kiroho Muhimu kwa Kazi ya Kupambana na Umaskini
A. Hali Yetu ya Kiroho ya Pamoja : tunakumbatia vipimo vifuatavyo vya hali ya kiroho ya pamoja:
1. Maisha ya Pamoja . Tunathibitisha na kushikilia ukweli kwamba utambulisho wetu (sisi ni nani) ni muhimu zaidi kuliko kile tunachofanya. Tunajitoa kwa kushiriki
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker