Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | MI ENENDO YA MA I SHA NA KAZ I YA KUPAMBANA NA UMASK I N I / 67
walengwa wetu; 2) kusaidia kwa njia ya ushirikiano; na 3) kujiwajibisha wenyewe ili kupata matokeo.
4. Kuzingatia Kalenda ya Kanisa . (1 Kor. 5:7). Kazi yetu ya kupambana na umaskini inatusukuma kutazama wakati kulingana na matukio. Tunaweza kushikwa mara kwa mara katika shida ya wakati huu.
Ukurasa wa 48 6
a. Badala ya kutazama wakati kulingana na matukio, tunautakasa wakati kwa kuunganisha hadithi yetu na hadithi ya Mungu.
b. Dhamira ya Msingi : Dhamiria kufuata majira ya kalenda ya kanisa na kusoma Maandiko ya kila wiki yanayohusu mada ya kila msimu.
c. Dhamira ya Juu : Dhamiria kufuata majira ya kalenda ya kanisa na kusoma Maandiko ya kila siku yanayohusu mada ya kila msimu.
5. Sabato . (Kum. 5:12-15; Mt 12:8). Kazi yetu ya kupambana na umaskini inaweza kutumeza kwa urahisi, na kutufanya tuwe watu wenye uraibu wa kazi bila kuwa na uwiano wowote kati ya kazi na maisha. Inaweza kutuibia utendaji wa akili kihisia zetu na uhai wa kimahusiano, na kuathiri afya yetu ya akili na ya kimwili.
Ukurasa wa 48 7
4
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
a. Badala ya kazi ya utetezi isiyokoma, tunafuata muundo wa kazi na kupumzika.
b. Dhamira ya Msingi : Dhamiria kutenga siku moja kamili kila wiki ili kupumzika kabisa pasipo kufanya kazi yoyote.
c. Dhamira ya Juu : Dhamiria kuwa na siku moja kamili ya kupumzika kwa wiki na siku kumi mfululizo kila mwaka ili kupumzika kabisa pasipo kufanya kazi.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker